Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu akisikiliza kwa
makini maelezo kutoka Mhandisi wa TTCL mkoa wa Ruvuma Abrahamu Msangi kuhusu
mtambo wa mawasiliano ya mnara huo wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati hiyo
(hawapo pichani) ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha
Mbatamila kilichopo wilayani Tunduru kwenye mkoani huo
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu (wa kwanza kushoto) akiongea na wananchi (hawapo pichani) wa kijiji cha Mbatamila kilichopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kuhusu umuhimu wa kulinda miundombinu ya mawasiliano wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano mkoani humo. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhandisi Ramo Makani na Mbunge wa jimbo la Tunduru Kaskazini akifafanua jambo kwa wananchi wa kijiji cha Mbatimila (wanaomsikiliza) kilichopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo (hawapo pichani) ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa huo
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu (wa kwanza kushoto) akiongea na wananchi (hawapo pichani) wa kijiji cha Mbatamila kilichopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kuhusu umuhimu wa kulinda miundombinu ya mawasiliano wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano mkoani humo. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhandisi Ramo Makani na Mbunge wa jimbo la Tunduru Kaskazini akifafanua jambo kwa wananchi wa kijiji cha Mbatimila (wanaomsikiliza) kilichopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo (hawapo pichani) ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa huo
NA WUUM, RUVUMA
KAMATI
ya Bunge ya Miundombinu imelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa
kujenga mazingira rafiki ya uwepo wa choo na kibanda cha mlinzi kwenye minara
ya simu iliyojengwa na Shirika hilo maeneo mbali mbali nchini kote
Hayo
yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa
Mchafu wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano
kwenye kijiji cha Mbatamila kilichopo kwenye kata ya Nampungu wilayani Tunduru
mkoani Ruvuma
Mhe.
Mchafu amesema kuwa tumeshuhudia kuwa Shirika letu la kizalendo la TTCL pekee
ndilo ambalo limejenga miundombinu rafiki ya choo na kibanda kwenye minara yao
yote waliyojenga kwenye maeneo mbali mbali nchi nzima kwa ajili ya mlinzi
anayelinda minara ya mawasiliano tofauti na kampuni nyingine za mawasiliano
ambapo zote kwa pamoja zimepatiwa ruzuku na Serikali kupitia Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ya kujenga minara hiyo kwenye maeneo yasiyo na
mvuto wa kibiashara
“Hongereni
mmepata mawasiliano ya mnara wa TTCL ambapo wamejenga miundombinu rafiki ya
choo na kibanda cha mlinzi cha kupumzikia hivyo mnara utalindwa muda wote,
kutakuwa hamna maambukizi ya magonjwa kwa kukosa choo”, amesema Mhe. Mchafu.
Ameipongeza TTCL kwa kuwa wamejenga mnara ambao unatoa mawasiliano muda wote
kwa kuwa kuna nishati ya jenereta kubwa ya kisasa.
Naye
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameipongeza
TTCL kwa kujenga minara ya mawasiliano yenye mazingira rafiki kwenye minara yao
yote iliyopo maeneo mbali mbali nchi nzima. Nditiye ameongeza kuwa Tunduru ni
Wilaya pekee ambapo TTCL ina jumla ya minara 14 na kupitia UCSAF itaongeza
minara mingine mitatu kwenye vijiji ambavyo vina mawasiliano hafifu kwa kuwa
lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanawasiliana. Ameongeza kuwa
Serikali inajenga meli na reli ya kisasa hivyo wahakikishe kuwa muda wote
wananchi wanawasiliana wakiwa safarini.Pia,
ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) kuhakikisha kuwa kampuni za simu zinatoa huduma ya mawasiliano
kwa wananchi ya kupiga simu, vifurushi na ujumbe kuendana na gharama ya vocha
iliyowekwa ambapo ni tofauti na TTCL ambao hawana ujaja ujanja wa kuwaibia
wananchi.
Akithibitisha
kuhusu upatikanaji wa mawasiliano mbele ya Kamati hiyo, mwananchi wa kijiji cha
Mabatamila kilichopo kwenye kata ya Nampungu iliyopo wilayani Tunduru mkoani
Ruvuma Bwana Kassim Zuberi amesema kuwa wanaipongeza TTCL kwa kutoa mawasiliano
kwa gharama nafuu zaidi ukilinganisha na kampuni nyingine za mawasiliano. “Tunaiomba
TTCL watufungulie huduma za 4G ili tuweze kupata mawasiliano ya intaneti”,
amesema Zuberi.
Mwendeshaji
wa UCSAF Mhandisi Albert Richard amesema kuwa UCSAF imetoa shilingi milioni 460
kwa TTCL ili iweze kujenga mnara huo ambapo wananchi wanapata mawasiliano. Pia,
ameongeza kuwa tayari UCSAF kupitia ruzuku inayotoa tayari minara 14 imejengwa
kwenye Wilaya hiyo na kwenye zabuni ijayo itaongeza minara mitatu ili wananchi
waweze kuwasiliana muda wote.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme akizungumza na wajumbe wa Kamati
hiyo walipofika ofisini kwake wakati wa ziara yao ya kukagua upatikanaji wa
mawasiliano mkoani humo, Mhe. Mndeme ameishukuru Serikali kwa kujenga minara 14
kwenye Wilaya ya Tunduru. Amesema kuwa mawasiliano ni kichocheo cha ukuaji wa
uchumi kwa kuwa wanapokea watalii wengi ambao wanachangia pato la taifa.
“Niwaombe watoa huduma watoe huduma ya intaneti kwa kuwa ni kikwazo kwa
wawekezaji mkoani kwetu ambapo wanataka wapate mawasiliano wakati wote,”amesema
Mndeme. Ameongeza kuwa mawasiliano yatasaidia miamala ya kifedha ambapo inakuwa
rahisi kwa wananchi kuwasiliana.
Pia,
amefafanua kuwa watoa huduma za mawasiliano wanaojenga minara waangalie
jiografia ya mkoa wa Ruvuma kwa kuwa una milima, misitu ni mingi sana, hifadhi,
mabonde, ziwa Nyasa na iko mpakani mwa nchi ambapo maeneo hayo yanakuwa na
changamoto za mawasiliano na baadhi ya maeneo ya Chiwindi na Chimati wananchi
hawapati mawasiliano. Amesema kuwa mawasiliano yanahitajika wakati wote hasa
maeneo ya mipakani kwa kuwa mawasiliano ni muhimu katika kuimarisha ulinzi na
usalama wa wananchi na taifa kwa ujumla
Mkuu
wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Albert Richard (wa pili
kushoto) akitoa maelezo kuhusu miundombinu rafiki ya mnara wa TTCL kwa Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu (wa tatu kushoto) wakati wa
ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha
Mbatamila kilichopo Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma. Wa pili kulia ni Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo
kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani) wakiwa ofisini
kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme (aliyekaa mbele) wakati wa
ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa huo
No comments :
Post a Comment