Tuesday, June 12, 2018

VIDEO:MATUKIO KATIKA PICHA HISTORIA ILIVYOANDIKWA TRUMP,KIM JONG UN WALIVYOKUTANA LIVE SINGAPORE




MKUTANO  wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani,  Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini,  Kim Jong Un,  umefanyika nchini Singapore.
Wawili hao walikutana kwanza kwa dakika 38 kwa mujibu wa Ikulu ya White House, na walikuwa ni wawili  pekee yao na wakalimani wao.

Mkutano huo ulianza kwa viongozi  hao wawili kusalimiana kwa tabasamu na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya Cappela Hotel kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana baina yao.
Rais Trump amesema wawili hao wamepiga hatua kubwa na kwamba karibuni kutakuwa na sherehe ya kutia saini nyaraka za makubaliano.

Wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia za kupunguza uhasama katika rasi ya Korea na kati ya Korea Kaskazini na Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia.
Hata hivyo, haijabainika ni nini kitakuwepo kwenye waraka ambao watautia saini. Trump alisikika akisema kuwa anatarijia makubaliano mazuri katika mkutano huku Kim akisema kuwa haikuwa rahisi kufika hapo.

Mkutano uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu naulifanyika katika Hotel ya Capella katika kisiwa cha utalii cha Sentosa.
Viongozi hawa wakiingia katika mkutano walionekana wenye tabasabu, na kusalimiana kwa kushikana mikono, na baadae Kim Jong Un alimshika bega Trumpa kisha wakaanza kuzungumza kwa msaada wa wakalimani wao.
Baadaye washauri na maofisa mbalimbali walitarajiwa kuingia kuendelea na mkutano huku suala la nyuklia likitarajiwa kujadiliwa kwa kina na haijajulikana bado makubaliano yatakuwa yapi.  Akizungumza kabla ya mkutano, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres,  amesema kuwa umoja huo utatoa msaada wowote wa kuhamasisha makubaliano katika mkutano huo.

”Viongozi wawili, wanajaribu kujadiliana jinsi ya kufikia makubaliano ambayo yalileta sana utata mwaka jana, amani na suala la kusitisha nyuklia ndiyo vinabaki kuwa lengo kuu, kama nilivyowaandikia mwezi uliopita kwamba kutahitajika ushirikiano wa hali ya juu na kutakuwa na changamoto za hapa na pale katika makubaliano, Marekani wanatakiwa kusimamia kwa vyovyote hali hiyo,” alisema Guterres.

Mkutano huu unaweza kuwa na mafanikio Uhusiano wa viongozi hawa wawili umepitia kwenye milima na mbonde kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita, wakirushiana matusi na kutishiana vita kabla ya uhusiano wao kuchukua mkondo mwingine na kuamua wawili hao kukutana.
Kwa nini hatua hii imefikiwa hivi sasa?
Mwaka wa kwanza wa Trump katika kiti cha urais ulianza kwa mvutano mkubwa na kurushiana maneno huku Kim naye akiendeleza majaribio ya silaha za nyuklia na kukiuka ilani ya kimataifa. Rais wa Marekani aliapa kupambana ikiwa Pyongyang ingeendelea kuitishia Marekani.

Korea Kaskazini iliendelea kukaidi na kufanya jaribio la nyuklia la sita mwezi Septemba mwaka 2017.
Baadaye Kim alitangaza kuwa nchi yake imefanikiwa katika mpango wake wa kuwa taifa la nyuklia, likiwa na silaha zinazoweza kuifikia Marekani.
Lakini mwanzoni mwa mwaka 2018, Korea Kaskazini ilianza kuboresha mahusiano na Korea Kusini kwa kupeleka timu na ujumbe kwenye michuano ya Olimpiki mjini Pyongyang.
Mwezi Machi, Donald Trump aliushangaza ulimwengu kwa kukubali mwaliko kutoka kwa Kim wa kukutana ana kwa ana.

Tangu wakati huo, njia ya kuelekea mkutano huu ikawa yenye changamoto ambapo Trump alikuwa akiahirisha kila mara kukutana huko.   Lakini hatimaye viongozi hao wamekaa pamoja. Singapore ni nchi ya tatu ambayo Kim Jong-un ameitembelea tangu alipokuwa kiongozi wa nchi yake mwaka 2011.
Safari yake ya kwanza ilikuwa nchini China mwezi Machi na mwezi Aprili akawa kiongozi wa kwanza wa Korea Kaskazini kutembelea Korea Kusini ambapo alikutana na Moon Jae-in.

No comments :

Post a Comment