Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman
Lamin akisaini kitabu cha wageni katika Zahanati ya Ololosokwan wilayani
Ngorongoro huku akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh.
Mrisho Gambo (kushoto) walipotembelea zahanati hiyo pamoja na mambo
mengine kuangalia ufanisi wake ambapo ziara hiyo iliambatana na hafla ya
Unesco kukabidhi kijiji digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani
Ngorongoro mkoani Arusha. Wengine ni kulia aliyeketi ni Naibu Katibu
Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Avemaria
Semakafu pamoja na na Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO
nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi ( wa pili kulia)
Kaimu
Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO nchini Tanzania, Dkt. Moshi
Kimizi (wa pili kushoto aliyeketi) akisaini kitabu cha wageni katika
Zahanati ya Ololosokwan kabla ya kuanza ziara fupi ya kutembelea kituo
hicho cha afya na kuangalia ufanisi wake ambapo ziara hiyo iliyoambatana
na hafla fupi ya Unesco kukabidhi kijiji digitali cha Ololosokwan kwa
serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Wengine katika picha ni Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo (kushoto), Naibu Katibu Mkuu Elimu
wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Avemaria Semakafu (kulia
aliyeketi) pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika
Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin (wa pili kulia).
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo akipata huduma ya matibabu kutoka
kwa Mtaalamu wa Magonjwa ya Kinywa wa Zahanati ya Ololosokwan, Dkt.
Godson Mbise wakati Mh. Gambo alipotembelea zahanati hiyo pamoja na
mambo mengine kuangalia ufanisi wake ambapo ziara hiyo iliyoambatana na
hafla fupi ya Unesco kukabidhi kijiji digitali cha Ololosokwan kwa
serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkurugenzi
wa Tehama MUHAS na Mratibu wa Huduma ya Tiba Mtandao, Dkt. Felix Sukums
(aliyeipa mgongo kamera) akibadilishana mawazo na Mganga Mkuu wa Wilaya
ya Ngorongoro, Dkt. Emmanuel Mallange (wa pili kushoto), Mwakilishi wa
Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin
(wa pili kulia) pamoja na Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO
nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi (kulia) nje ya jengo la huduma ya
kinywa katika zahanati ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkurugenzi
wa Tehama MUHAS na Mratibu wa huduma ya tiba mtandao, Dkt. Felix Sukums
(kulia) akibainisha changamoto zinazoikabili kitengo cha ‘Ultra Sound’
katika Zahanati ya Ololosokwan kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho
Gambo (wa pili kushoto) wakati wa ziara fupi ya kutembelea kituo hicho
cha afya cha kijiji cha digitali na kuangalia ufanisi wake ambapo ziara
hiyo iliambatana na hafla ya Unesco kukabidhi kijiji digitali cha
Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Wengine ni
Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO nchini Tanzania, Dkt. Moshi
Kimizi, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki
ofisi ya Nairobi, Bw. Abdul Rahman Lamin pamoja na Mganga Mkuu wa Wilaya
ya Ngorongoro, Dkt. Emmanuel Mallange (wa pili kushoto).
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo (wa tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya
ya Ngorongoro, Mh. Rashid Mfaume Taka (wa pili kushoto), Diwani wa kata
ya Ololosokwan, Mh. Yannick Ndoinyo (kushoto), pamoja na Naibu Katibu
Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Avemaria
Semakafu (kulia) na ujumbe ulioambatana na Mh. Gambo wakikagua ujenzi wa
nyumba za watumishi wa zahanati ya Ololosokwan zinazojengwa na wananchi
wa Ololosokwan wakati wa ziara fupi ya kutembelea kituo hicho cha afya
na kuangalia ufanisi wake iliyoambatana na hafla ya Unesco kukabidhi
kijiji digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani
Arusha.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo (kushoto) akiwa ameambatana na
Ofisa Programu Msaidizi wa Unesco, Hamidun Kweka mara baada ya kuwasili
eneo la tukio wakielekea kukagua shule ya mtandao inayotumia umeme wa
jua kabla ya kuelekea kwenye hafla ya Unesco kukabidhi kijiji digitali
cha Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman
Lamin (kulia) na Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO nchini
Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi wakiwasili kwenye eneo la tukio la Unesco
kukabidhi kijiji digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani
Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkuu
wa Wilaya ya Ngorongoro, Mh. Rashid Mfaume Taka (wa tatu kulia)
akijadiliana jambo na Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith
Shayo (kushoto) kuhusiana na protokali kabla ya kuanza hafla ya
makabdhiano ya kijiji cha digitali cha Ololosokwan baina Serikali na
Unesco wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mwanafunzi
Rehema Lucas wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Emanyata akitoa
maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo na Mwakilishi wa
Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin
(hawapo pichani) kuhusu program ya masomo mbalimbali ikiwemo somo la
Biology inayopatika ndani ya kompyuta mpakato (laptop) katika shule ya
mtandao inayotumia umeme wa jua kabla ya kuelekea kwenye hafla ya Unesco
kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani
Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa
UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin pamoja na
wanafunzi wa shule ya sekondari Emanyata wanaonufaika na kijiji cha
digitali cha shule ya mtandao inayotumia umeme wa jua wakimsikiliza
Mwanafunzi Rehema Lucas (hayupo pichani) kabla ya kuelekea kwenye hafla
ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali
wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Ofisa
Programu Msaidizi wa Unesco ambaye pia ni Mratibu wa kijiji cha
digitali, Hamidun Kweka akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh.
Mrisho Gambo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika
Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin kuhusiana na kijiji cha digitali cha
shule ya mtandao inayotumia umeme wa jua kabla ya kuelekea kwenye hafla
ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali
wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa
UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin wakitoka ndani
ya kijiji cha digitali cha shule ya mtandao inayotumia umeme wa jua
kuelekea kwenye hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha
Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo na ujumbe wake wakipata maelezo
kutoka kwa Ofisa Programu Msaidizi wa Unesco, Bw. Hamidun Kweka kuhusu
shughuli mbalimbali zinazofanywa na jamii ya wamasai katika kituo cha
mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni cha jamii ya wamasai (Community
Arts Space-CAS) kilichojengwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ushirikiano wa
Unesco kwenye kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman
Lamin (kulia) akijaribu moja ya bidhaa za shanga zinazotengenezwa na
wakinamama wa kimasai katika kituo cha mafunzo ya kazi za mikono na
utamaduni cha jamii ya wamasai (Community Arts Space-CAS) kilichojengwa
na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ushirikiano wa Unesco kwenye kijiji cha
Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha huku Kaimu Mkuu wa Ofisi
za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akionyesha moja ya bidhaa
iliyotengenezwa kwa shanga na kuandikwa UNESCO.
Kaimu
Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akiteta jambo na
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul
Rahman Lamin wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha
Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Wengine
meza kuu kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro,
Emmanuel Sukums pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mh. Rashid
Mfaume Taka.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo akizungumza na wananachi wa kijiji
cha Ololosokwan pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa
hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa
serikali, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman
Lamin akizungumza kwa niaba ya Ann Therese Ndong-Jatta wakati wa hafla
ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali
iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani
Arusha.
Naibu
Katibu Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi.
Avemaria Semakafu akitoa salamu za Wizara ya Elimu pamoja na za Mbunge
wa Jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo,Ufugaji na
Maendeleo ya Uvuvi, Mh. William Ole Nasha wakati wa hafla ya Unesco
kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika
katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkurugenzi
wa Tehama MUHAS na Mratibu wa huduma ya tiba mtandao, Dkt. Felix Sukums
akitoa salamu za MUHAS wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha
digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha
Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Diwani
wa kata ya Ololoskwan, Mh. Yannick Ndoinyo akitoa neno la shukran kwa
niaba ya wananchi wake kwa mgeni rasmi na Unesco kwa ushiriki wao wakati
wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa
serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro
mkoani Arusha.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Abudl Rahman Lamin (wa tatu kushoto) akimwakilisha Ann Therese Ndong’
Jatta, Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki akimkabidhi rasmi
ripoti ya mradi wa kijiji cha kidigitali (Unesco-Samsung Digital
Village) kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mh. Rashid Mfaume Taka (wa
tatu kulia) kwa ajili ya uendelezaji baada ya majaribio wakati wa hafla
iliyofanyika katika kituo cha mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni cha
jamii ya wamasai (Community Arts Space-CAS) kilichojengwa na Umoja wa
Ulaya (EU) kwa ushirikiano wa Unesco kwenye kijiji cha Ololosokwan
wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo Naibu Katibu Mkuu Elimu wa
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Avemaria Semakafu
(waliosimama kwa nyuma), Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini,
Faith Shayo (kushoto), Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO
nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi (wa pili kushoto), Diwani wa kata ya
Ololosokwan, Mh. Yannick Ndoinyo (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa
Kitongoji cha Ololosokwan, John Pyando (kulia).
Kikundi
cha wakinamama wakimasai wakitoa burudani kwa wageni waalikwa wakati wa
hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa
serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro
mkoani Arusha.
Baadhi
ya wanakijiji wa Ololosokwan waliohudhuria hafla ya Unesco kukabidhi
kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika
kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Baadhi
ya wazee wa kijiji cha Ololosokwan waliohudhuria hafla ya Unesco
kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika
katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman
Lamin akipokea zawadi ya Mbuzi kutoka kwa wakinamama wa kimasai
wanaofanya shughuli zao katika kituo cha mafunzo ya kazi za mikono na
utamaduni cha jamii ya wamasai (Community Arts Space-CAS) kilichojengwa
na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ushirikiano wa Unesco kwenye kijiji cha
Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Kushoto ni Kaimu Katibu
Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi.
Kaimu
Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akipokea zawadi kutoka
kwa Mwakilishi wa kikundi cha wakinamama wakimasai wanaofanya shuhghuli
zao katika kituo cha mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni cha jamii
ya wamasai (Community Arts Space-CAS) kilichojengwa na Umoja wa Ulaya
(EU) kwa ushirikiano wa Unesco kwenye kijiji cha Ololosokwan wilayani
Ngorongoro mkoani Arusha. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa
wa UNESCO nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi.
Naibu
Katibu Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi.
Avemaria Semakafu akivalishwa zawadi ya hereni zilizotengenezwa na
wakinama wa kimasai wanaojishughulisha katika kituo cha mafunzo ya kazi
za mikono na utamaduni cha jamii ya wamasai (Community Arts Space-CAS)
kilichojengwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ushirikiano wa Unesco kwenye
kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Na Mwandishi wetu,
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wamekabidhi
rasmi kijiji cha digitali cha Ololosokwan katika sherehe kubwa
iliyofanyika kijijini hapo na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali na
mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Katika kukabidhiana huko Unesco imesema kwamba itaendelea kutoa msaada katika mtandao wa intaneti kwa miezi sita ijayo.
Katika
hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na Dk. Abdul Rahman Lamin, Ofisa
msimamizi wa ofisi ya Unesco, Ann Therese Ndong-Jatta alisema kwamba
wakati wanakabidhi facility hizo wamefurahishwa na ushirikiano mkubwa
waliopewa katika mradi huo.
Kijiji
cha digitali cha Ololosokwan ni moja ya vijiji vinne ambavyo
vimefadhiliwa huku vikitoa huduma muhimu za elimu, afya na biashara
kuendeshwa kidigitali.
Kijiji
hicho cha digitali ambacho ni matokeo ya ushirikiano kati ya UNESCO na
kampuni ya Samsung imelenga kutoa elimu kwa kutumia njia ya mtandao,
kufaniklisha tiba mtandao na pia kutumia mtandao wa kompyuta katika
kuwezesha biashara.
Ofisa
huyo alisema kuna haja ya kuendeleza ushirikiano uliopo ili mradi uweze
kuendelea kuchangia maendeleo ya wakazi wa eneo hilo.
Aidha
aliitaka serikali kuhakikisha kwamba inaendeleza ushawishi kwa wananchi
wa eneo hilo la Ngorongoro kutumia vyema teknolojia ya kisasa katika
kufanikisha maisha endelevu ya zana zilizopo.
“UNESCO
inajisikia furaha kwa kutambua kwamba kupitia mradi wa kijiji cha
digiti, wilaya ya Ngorongoro imekuwa miongoni mwa waanzizilishi wa
matumizi ya Tehama katika kufanikisha elimu na afya nchini Tanzania. “
alisema Ndong-Jatta .
Alisisitiza
kuwa kuwapo kwa kijiji hicho kunaambatana na mamchakato wa sasa wa
serikali ya awamu ya tano ya kuwa na taifa lenye uchumi wa kati ifikapo
mwaka 2025.
“Nataka
kuhakikishia wilaya ya Ngorongoro, kijiji cha Ololosokwan na serikali
ya Tanzania kwamba UNESCO itaendelea kutoa msaada wa kiufundi na
kuhakikisha kwamba kunakuwa na maendeleo endelevu kwa kijiji hichi”
alisema Ndong-Jatta.
Akipokea
mradi huo Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo alisema kwamba
serikali ina mipango endelevu ya kuhakikisha kwamba kijiji hicho
kinaendelea kuwa cha mfano.
Alisema kijiji hicho kitapitiwa na umeme ili kuongeza nguvu ya nishati iliyopo sasa inayotegemea umeme jua.
Aidha
alisema kwamba serikali imefurahishwa na mradi huo ambao umelenga
kusaidia wananchi wa eneo hilo hasa katika afya, uchumi na elimu.
Alisema
eneo hilo linachangamoto kubwa kutokana na utamaduni wa wafugaji wa
kimasai ambapo elimu ya watoto wote wakiwamo wa kike .
Alisema
wataendelea kukabiliana na changamoto zilizopo za wafugaji katika elimu
kuhakikisha kwamba watoto wa kimasai wanapata elimu pamoja na tabia
iliyopo ya uhamaji.
Pia
alisema wapo tayari kushirikiana na watu wote wanaotaka kusaidia
maendeleo ya Tanzania kwa kuzingatia matakwa ya nchi ya maendeleo.
Alishurukuru
Unesco na Samsung kwa kusaidia jamii ya ufugaji kufanya zaidi ya kufuga
Ng’ombe hasa kwa kuhakikisha kila kitu katika Ng’ombe kuna kazi zao.
Alishukuru
kwa kusaidia kuwepo kwa utaalamu wa kutengeneza vifaa vya kitalii kwa
kuwa na eneo la kisasa lenye bidhaa za kitamaduni zinazochangia kukuza
uchumi wa Ololosokwan.
Naye
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Mh. Rashid Taka alisema kwamba
anashukuru kuwapo kwa mradi huo na kwamba wameupokea mradi na kuahidi
kuufanya kuwa endelevu.
Alisema
kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa ni mali ya jamii na kwamba uongozi wa
wilaya utaweka macho kuhakikisha kwamba uendeshaji wa kijiji unakwenda
unavyostahili kuwa.
Naye
Dkt. Felix Sukums wa MUHAS amesema kwamba wataendelea kuboresha huduma
ya afya kwa njia ya mtandao kwa kutoa huduma masafa na ushauri wa
kitaalamu kwa njia ya mtandao mara tu tatizo la mtandao litakapomalizwa
kwa kushirikiana na UNESCO tiba mtandao
Naye
Naibu Katibu Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia,
Avemaria Semakafu ameshukuru kwa Unesco kukabidhi kijiji cha digitali na
kulitaka shirika hilo kusaidia elimu ya watu wazima kwa kutumia kituo
hicho.
Amesema kwamba wizara ya elimu imejifunza mno kuhusu teknolojia inavyoweza kutumiwa katika elimu ya masafa.
Anasema kijiji hicho kimefunza mengi kutokana na mafanikio makubwa yanayoonekana katika matumizi ya teknolojia.
No comments :
Post a Comment