Msimamizi wa Fedha Tamisemi Bi
Ummy Wayayu(kushoto) akijadili jambo mara baada ya ufunguzi wa mafunzo
ya siku nne ya Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (Epicor 10.2)
yanayoendelea yaliyoanza mkoani mtwara na kushirikisha wahasibu,waweka
hazina na maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa ya Pwani,Mtwara, kinondoni
manispaa na Ruvuma…Katikati ni Hafidh Issa,Mweka hazina Kisarawe na
Suzan Chaula Mweka hazina Halmashauri ya mji wa Kibaha Mkoani Pwani
Kiongozi wa
timu ya mifumo ya fedha katika mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta
za Umma PS3, Dokta Gemini Mtei, akitoa somo kwa washiriki wa mafunzo ya
matumizi ya mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (EPICOR 10.2),
yanayoendelea mkoani Mtwara yakishirikisha wahasibu na waweka hazina wa
halmashauri za mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara na Ruvuma. Mafunzo
ambayo yanaendeshwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI chini ya mradi wa PS3
unaofadhiliwa na shirika la Kimarekani la USAID.
Baadhi ya
washiriki wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa usimamizi wa fedha za umma
(EPICOR 10.2), yanayoendelea mkoani Mtwara yakishirikisha wahasibu na
waweka hazina wa halmashauri za mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara na
Ruvuma, wakifuatilia somo. Mafunzo ambayo yanaendeshwa na Ofisi ya Rais
TAMISEMI chini ya mradi wa PS3 unaofadhiliwa na shirika la Kimarekani
la USAID.
Mhasibu wa manispaa ya Kinondoni
jijini Dar es Salaam, Pendo Sangija (kushoto) na Mweka hazina wa
halmashauri ya mji wa Nanyamba mkoani Mtwara, wakifuatilia somo kutoka
kwa wawezeshaji wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa usimamizi wa fedha za
umma (EPICOR 10.2), yanayoendelea mkoani Mtwara yakishirikisha wahasibu
na waweka hazina wa halmashauri za mikoa ya Dar es Salaam, Pwani,
Mtwara na Ruvuma. Mafunzo ambayo yanaendeshwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI
chini ya mradi wa PS3 unaofadhiliwa na shirika la Kimarekani la USAID.
………………..
Na ABDULAZIZ AHMEID -MTWARA
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana naMradi wa Uimarishaji wa
Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) wanaendelea natoa mafunzo ya kina kwa
watumishi wa kada ya uhasibu kutoka mamlaka 185 za Serikali za Mitaa
Tanzania.
Akifungua mafunzo hayo yanayohusu
mfumo mpya wa Epicor 10.2, leo katika manispaa ya Mtwara ,Afisa
msimamizi wa mifumo ya fedha Tamisemi,Bi Ummy Wayayu amesema mafunzo
hayo ya mfumo wa Epicor yamelenga kuwapa uelewa Wahasibu juu ya
mabadiliko ya maboresho makubwa yaliyofanywa katika mfumo huo.
Mafunzo hayo yanaendeshwa kutokana
na Halmashauri nchini kuanza matumizi ya mfumo katika toleo
lililojulikana kama Platnum mwaka 1999/2000 na baadaye mfumo ulifanyiwa
maboresho na kufungwa epicor toleo Na 7.2 mwaka 2001 wakati huo mfumo
ukiwa umefungwa katika Halmashauri 38 pekee
Na ilipofika mwaka 2014/15 mfumo
uliboreshwa na kuwa epicor toleo la 7.3.5 na kufungwa katika Halmashauri
44 zaidi hivyo kuwa na Jumla ya Halmashauri 82zilizokuwa zinatumia
mfumo na hadi kufikia july Mwaka 2012, TAMISEMI ilifanya maboresho
makubwa kwa kuunganisha Halmashauri 133 zilizokuwepo wakati huo
kupitia kampuni ya simu ya taifa TTCL na kuweka epicor toleo namba 9.05
ambalo limeendelea kutumika hadi sasa.
Hata hivyo Halmashauri
zilizoongezeka baadaye zilifungwa epicor toleo namba 10.1 ambalo
limeboreshwa sasa na kuwa 10.2 inayofungwa Halmashauri zote zimeanza
matumizi ya epicor toleo namba 10.2 ambayo ni hatua kubwa sana katika
utekelezaji wa dhana nzima ya uwazi uwajibikaji na utawala bora katika
usimamizi wa fedha za umma.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki
akiwemo mweka hazina wa Halmashauri ya Bagamoyo,kibaaha na kisarawe
mkoani Pwani walibainisha kuwa mfumo huo utasaidia Halmashauri
kuondokana na vyeti vya hati chafu na zile zenye mashaka kutokana na
mapato na matumizi ya fedha zote kutakiwa kuingizwa katika mfumo huo.
Aidha walibainisha kuwa uboreshaji
wa mfumo wa Epicor ni muendelezo wa uboreshaji wa mifumo ya Serikali
kama ilivyofanyika kwa mifumo mingine kama vile mifumo ya Afya.
Maboresho mengine yaliyofanyika
katika mfumo huo wa Epicor 10.2 ni kwamba mifumo yote ya msingi ya
usimamizi wa fedha katika sekta za umma kwa sasa itaweza kuwasiliana na
kushirikishana taarifa ambapo hapo awali, uongozi na maafisa katika
Mamlaka za Serikali za Mitaa walilazimika kupitia mipango na bajeti
katika mfumo mmoja, mapato katika mfumo mwingine na matumizi kwenye
mfumo mwingine, hivyo kuleta ugumu katika kudhihirisha uwajibikaji,
ufanisi na thamani ya fedha katika matumizi ya fedha za Serikali.
Sambamba na kutumika kwa mfumo huo
ambao utaunganishwa na mfumo unaowezesha mabenki kulipana Tanzania
(TISS) ambao utaruhusu malipo yote kufanyika kwa njia ya kielektroniki.
Mafunzo hayo yanafanyika katika
vituo sita ambavyo ni Dodoma,Mwanza, Mtwara, Iringa, Kagera na Mbeya
yakijumuisha watumiaji wa mfumo huo ambao ni Waweka Hazina na Wahasibu
na baadaye Maafisa TEHAMA, Maafisa Manunuzi na Wakaguzi wa Ndani na
kuendeshwa na PS 3 kwa usimamizi wa Tamisemi na kufadhiliwa na USAID
Washiriki waliopewa mafunzo
kupitia kituo cha kanda ya mtwara ni pamoja na mikoa ya
Lindi,Mtwara,Ruvuma na sasa ni Pwani Dar es sallam na baadhi ya wilaya
za mkoa wa mtwara
No comments :
Post a Comment