Monday, June 11, 2018

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MRATIBU MKAZI WA MASHIRIKA YA UN NCHINI


Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Prof. Adolf Mkenda (kulia) akizungumza na 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez alipofika
Wizarani tarehe 11 Juni, 2018 kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Serikali ya Tanzania pamoja na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) hapa nchini. Kwa upande wake, Prof. Mkenda alipongeza Mpango wa One UN unaotekelezwa na Ofisi za Umoja wa Mataifa hapa nchini kwa vile unarahisisha utekelezaji wa majukumu na kushukuru ushirikiano mzuri uliopo kati ya Umoja wa Mataifa na Tanzania hususan katika program za kupunguza umaskini na maendeleo endelevu.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimatifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy akiwa na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Eva Ng’itu wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof.
Mkenda na Bw. Rodriguez hawapo pichani
Bw. Rodriguez nae akimweleza jambo Prof. Mkenda
Mazungumzo yakiendelea
Picha ya pamoja

No comments :

Post a Comment