Saturday, June 30, 2018

DStv NA UBER WAJA NA OFA KABAMBE!


Kampuni za MultiChoice Tanzania na UBER zimetangaza ushirikiano maalum ambapo kwa sasa madereva wa UBER wanaweza kuwa mawakala wa DStv na na pia wateja wa DStv kupata punguzo maalum kwa safari zao kutumia UBER.
Katika ushirikiano huo, medereva wote wa UBER wataweza kupata seti ya DStv kwa shilingi 69,000 tu pamoja na kifurushi cha mwezi mmoja bure.
Kwa wateja wa DStv ambao wanapakua App ya UBER kwa mara ya kwanza watapata punguzo la shilingi 6,200 kwa safari yao ya kwanza na UBER
1
Afisa Mauzo wa MultiChoice Tanzania Gloria Anderson (katikati) akiongea wakati wa hafla ya kutangaza ushirikiano kati ya DStv na UBER utakaowawezesha wateja wa DStv kupata punguzo maalum wanapotumia usafiri wa UBER na pia madereva na wafanyakazi wa UBER kupata ofa maalum wananuapo DStv.
2
Mkuu wa Mawasiliano wa MultiChoice TanzaniaJohnson Mshana (Kulia) akiongea wakati wa hafla ya kutangaza ushirikiano kati ya DStv na UBER utakaowawezesha wateja wa DStv kupata punguzo maalum wanapotumia usafiri wa UBER na pia madereva na wafanyakazi wa UBER kupata ofa maalum wananuapo DStv. Kutoka kushoto ni Afisa Masoko wa MultiChoice Gloria Anderson, Balozi maalum wa DStv Nancy Sumari na Afisa muandamizi wa UBER Davis Evans
3
Balozi maalum wa DStv Nancy Sumari akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Muandamizi wa UBER Davis Evans
4
Afisa muandamizi wa UBER Davis Evans akitoa maelezo kuhusu ushirikiano kati yao na DStv. Katikati ni balozi maalum wa DStv Nancy Sumari na kushoto ni Afisa Mauzo wa MultiChoice Tanzania Gloria Anderson.

No comments :

Post a Comment