Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage (katikati) akieleza jambo wakati
alipokutana na ujumbe kutoka Ubalozi wa Jumuiya ya Ulaya kujadiliana
Taarifa ya Utazamaji wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 iliyotolewa na
jumuiya hiyo.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mkuu Mst. (Znz)
Hamid Mahmoud Hamid na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mkuu wa
Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Giveness Aswile.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage (wa nne kushoto) akifafanua
jambo kwa Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) Roeland Van de Geer (wa pili
kushoto) na Mtaalau wa Masuala ya Siasa wa EU, Anna Costantin.Ujumbe huo
ulifika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam kujadili Taarifa ya
Utazamaji wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ilyotolewa na jumuiya hiyo.
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Asina Omari (wa pili kulia) akiwasilisha taarifa fup
kuhusu Tume na majukumu yake kwa ujumbe kutoka Ubalozi wa Jumuiya ya
Ulaya (EU) (kushoto) uliofika ofisi za NEC kujadili Taarifa ya Utazamaji
wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 iliyotolewa na jumuiya hiyo.Katikati ni
Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage.
Picha na Hussein Makame-NEC
No comments :
Post a Comment