Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa
Kampeni ya Elimu na Usajili wa Walipakodi Mjini Bariadi, ambayo
inaendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani humo.
Kamishna Mkuu TRA , Bw. Charles
Kichere akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Serikali pamoja na
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu, wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya
Elimu na Usajili wa Walipakodi Mkoani humo ambao umefanyika Mei 08,
Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa
Mlipakodi TRA Bw. Richard Kayombo akizungumza na Viongozi na Watendaji
wa Serikali pamoja na Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu, wakati wa
Uzinduzi wa Kampeni ya Elimu na Usajili wa Walipakodi Mkoani humo ambao
umefanyika Mei 08, mjini Bariadi.
Katibu wa Chama cha
Wafanyabiashara(TCCIA) Mkoa wa Simiyu, Bibi. Christina Matulanya
akichangia hoja mbele ya wafanyabiashara wenzake wakati wa Uzinduzi wa
Kampeni ya Elimu na Usajili wa Walipakodi Mkoani humo ambao umefanyika
Mei 08, mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Serikali pamoja
na Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu, wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya
Elimu na Usajili wa Walipakodi Mkoani humo ambao umefanyika Mei 08,
mjini Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,
Bw.Jumanne Sagini akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Serikali
pamoja na Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu, wakati wa Uzinduzi wa
Kampeni ya Elimu na Usajili wa Walipakodi Mkoani humo ambao
umefanyikaMei 08, mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa TRA kuhusu namna
Wafanyabiashara watakavyokuwa wakisajiliwa , mara baada ya Uzinduzi wa
Kampeni ya Elimu na Usajili wa Walipakodi Mkoani humo ambao umefanyika
Mei 08 Mjini Bariadi.
Mfanyabiashara Gungu Emmanuel
Silanga akichangia hoja mbele ya wafanyabiashara wenzake wakati wa
Uzinduzi wa Kampeni ya Elimu na Usajili wa Walipakodi Mkoani Simiyu
ambao umefanyika Mei 08, mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Chama cha
Wafanyabiashara Wilaya ya Busega, Bw.Davis Mateko akichangia hoja mbele
ya wanyabiashara wenzake wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Elimu na
Usajili wa Walipakodi Mkoani Simiyu ambao umefanyika Mei 08, Mjini
Bariadi.
………………
Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
inatarajia kuanzisha vituo vya Elimu na huduma kwa walipakodi hivi
karibuni, ambavyo vitawasaidia walipakodi kupata ushauri wa masuala ya
kodi pamoja na kujua haki na wajibu wao.
Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania Charles Kichere Mjini Bariadi, wakati
akizungumza na wafanyabiashara, Viongozi na watendaji wa Wilaya na Mkoa
Mkoani Simiyu, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Elimu na Usajili kwa
Walipakodi mkoani humo.
Kamishna Kichere amesema uamuzi wa
TRA wa kuanzisha vituo hivyo umelenga kusogeza huduma karibu kwa
walipakodi, ambapo wafanyabiashara(walipakodi) watapata huduma za
ushauri kuhusu masuala ya kodi bila malipo katika vituo hivyo
vitakavyokuwa nje ya Ofisi za TRA.
“Tunajua elimu ni muhimu sana kwa
walipakodi wetu, tunataka itolewe kwa walipa kodi kila siku siyo kwa
misimu; ili kusogeza huduma karibu hivi karibuni tutaanzisha vituo vya
Elimu na Huduma kwa walipakodi nje ya TRA, ambavyo vitatoa huduma ya
ushauri kwa walipakodi bure” alisema Kichere
Aidha, Kichere ametoa wito kwa
Wafanyabishara wa Mkoa wa Simiyu ambao ameutaja kama mkoa wenye fursa
nyingi za kibiashara kujitokeza kwa wingi kujisajili katika vituo vya
elimu na usajili wa walipakodi, kupitia zoezi linaloendelea mkoani humo
ambalo limezinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka, Mei
08, 2018.
Ameongeza kuwa ni vema
wafanyabiashara wakatambua umuhimu wa kulipa kodi stahiki kwa wakati
stahiki, ili Serikali iendelee kutoa huduma bora kwa wananchi kupitia
kodi hizo na akasisitiza wafanyabiashara ambao bado hawajarasimisha
biashara zao wajisajili na kuanza kulipa kodi .
Wafanyabishara wa Mkoa wa Simiyu
wameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Simiyu kwa kufanya nao
kazi kwa ushirikiano na wakaomba changamoto mbalimbali zilizopo
kufanyiwa kazi ili waweze kutimiza wajibu wao kikamilifu kama
walipakodi.
“ Tunaomba Ofisi ya Mkoa ya TRA
iboreshwe iendane na hadhi ya Mkoa, Wilaya zetu mpya za Busega na
Itilima ziwe na Ofisi za TRA ili kuwaondolea wafanyabiashara wenzetu
shida ya kufuata huduma katika wilaya nyingine na pia wafanyabiashara
tunahitaji elimu ya mara kwa mara kwenye masuala ya kodi” alisema
Christina Matulanya Katibu wa TCCIA Simiyu.
“Tunaomba TRA waziangalie upya
sheria zao, lakini pia waangalie viwango vya kodi wanavyowakadiria
wafanyabiashara ili viendane na hali halisi ya biashara za Watanzania
tulio wengi” alisema Davis Mateko Mfanyabiashara kutoka Wilaya ya
Busega.
Akizindua kampeni ya Elimu na
Usajili kwa walipakodi , Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka
ameiomba TRA kutatua changamoto za mashine za kutolea risiti (EFD), huku
akitangaza dhamira yake ya kuona biashara zinafanyika saa 24 katika
Makao Makuu ya Wilaya na Baadhi ya Vituo (Centres) vikubwa kuiwezesha
TRA kukusanya kodi zaidi.
Katika hatua nyingine Mtaka
amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri Mkoani humo kutekeleza agizo la
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
la kuzingata maeneo ya wafanyabiashara wadogo wakati wa Ujenzi wa Vituo
vya Mabasi na akasisitiza wafanyabiashara wadogo kujisajili ili waweze
kupewe kipaumbele vituo hivyo vitakapojengwa
No comments :
Post a Comment