Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani
Kikwete (CCM) akielezea shughuli za uchimbaji wa madini ya kokoto kwa
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko na wananchi wa wilaya ya Bagamoyo
(hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika katika eneo la Lugoba
wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Sehemu ya wakazi wa eneo la Lugoba
lililopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wakifuatilia ufafanuzi
uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo
pichani)
Mchimbaji kutoka kampuni ya Gulf
Concrete and Cement Products, Augustine Modest akiwasilisha kero yake
kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) katika mkutano
huo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto
Biteko akinukuu maswali mbalimbali yaliyokuwa yanaulizwa na wachimbaji
madini ya kokoto (hawapo pichani) katika mkutano huo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto
Biteko akitoa ufafanuzi wa maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wananchi
mbalimbali walioshiriki katika mkutano huo.
……………….
Naibu Waziri wa Madini, Doto
Biteko leo tarehe 06 Mei, 2018 amekutana na wachimbaji wa madini ya
ujenzi aina ya kokoto katika eneo la Lugoba wilayani Bagamoyo mkoani
Pwani. Mkutano huo uliohusisha Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mbunge wa
Chalinze, Ridhiwani Kikwete na wananchi, ulilenga kujadili changamoto
katika uchimbaji madini ya ujenzi aina ya kokoto.
Katika mkutano huo, Naibu Waziri
Biteko alitoa maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na wawekezaji
kuendeleza maeneo yao, wawekezaji kutouza leseni kwa mtu mwingine
pasipo kushirikisha serikali, wawekezaji kuandaa mpango wa utoaji huduma
kwa jamii pamoja na kuutekeleza na Ofisi ya Madini ya Kanda ya
Mashariki kufuatilia ahadi za wawekezaji katika huduma za jamii na
kuwasilisha ripoti mara moja.
Maelekezo mengine ni pamoja na
Ofisi ya Madini Kanda ya Mashariki kuwasilisha ripoti ya athari za
mazingira kabla ya Mei 20, 2018, wawekezaji kushirikiana na wananchi
wanaowazunguka, kampuni zenye mgogoro na wananchi kuhakikisha zinamaliza
tofauti zao na fedha za halmashauri kutumika kwenye uwekezaji mwingine
kwa ajili ya maendeleo.
No comments :
Post a Comment