Wednesday, May 2, 2018

Muhimbili, MUHAS Watoa Mafunzo Ya Awali kwa Watoa Huduma Wa Magonjwa Ya Dharura


0001
Dkt. Olivia  Rusizoka ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Hedwiga Swai akifunga mafunzo ya siku tano yaliowashirikisha wataalamu wa afya wa Magomjwa ya Dharura na Ajali kutoka manispaa tano za Jiji la Dar es Salaam ambayo yaliandaliwa na Muhimbili, EMAT na MUHAS . Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga na Dkt. Upendo George wakiwa kwenye mkutano wa kufunga mafunzo hayo.
002
Wataalamu wa kutoa huduma za magonjwa  ya Dharura na Ajali wakiwa kwenye mkutano wa mafunzo ya nadharia na vitendo ambayo yamefungwa na Dkt. Rusizoka aliyemuwakilisha Mkurugenzi wa Tiba,  Dkt. Hedwigwa Swai.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali wa Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga akisisitiza madhumuni na umuhimu wa kuendesha mafunzo hayo. Kulia ni Dkt. Rusizoka na Dkt. Upendo.
004
Wataalamu  wanaotoa huduma ya  magonjwa ya  Dharura na Ajali wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo.
005
Mmoja wa wataalamu wa kutoa huduma za Magonjwa ya Dharura na Ajali, Fatma Chichiri akipokea cheti kutoka kwa Dkt. Rusizoka.
????????????????????????????????????
Mmoja wa wataalamu wa huduma hizo, Buheri Kiberiti akikabidhiwa cheti baada ya kukamilika  kwa mafunzo hayo.
007
Mtaalamu wa kutoa huduma za magonjwa  ya Dharura na Ajali, Tuma Kanyumbu akipokea cheti kutoka kwa Dkt. Rusizoka. Kushoto ni Msimamizi wa mafunzo hayo,  Dkt. Patrick Shayo,  Dkt. Juma Mfinanga, Dkt. Rusizoka na Dkt. Upendo Geonge.
008
Wataalamu wa kutoa huduma za magonjwa ya  Dharura na Ajali wakiwa kwenye picha ya pamoja  na wakufunzi  wao baada  ya mafunzo kufungwa na Dkt. Rusizoka.
JOHN STEPHEN, Hospitali ya Taifa Muhimbili
…………………..

Wataalamu Bingwa wa Huduma ya Tiba ya Dharura na Ajali wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba Shirikishi(MUHAS)kwa kushirikian na
Chama cha Wataalamu wa Magonjwa ya Dharura na Ajali Tanzania (EMAT) wameendesha mafunzo ya awali kwa watoa huduma kuhusu ya magonjwa ya dharura na ajali.
Mafunzo hayo ya siku tano yalifanyika kwa watumishi 16 wanaotoka katika  hospitali za rufaa katika Manispaa tano za Mkoa wa  Dar es Salaam, wakiwamo waaguzi saba, afisa wauguzi  wanne,  tabibu wasaidizi watatu, Madaktari wasaidizi watatu na daktari mmoja.
Mafunzo hayo yalilenga watoa huduma ambao wamekuwa wakifanya kazi kwenye  magari ya
wagonjwa (Ambulance) katika Mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni maandalizi ya kozi ya wiki sita inayotegemewa kufundishwa na MUHAS kwa kushirikiana na  Idara ya Magonjwa ya Tiba ya Dharura na Ajali ya Muhimbili kwa watoa huduma wa ambulance Tanzania.
Katika mafunzo hayo, wanafunzi walifundishwa mafunzo ya  nadharia na vitendo kwa baadhi ya mada ambazo zinatarajiwa kutolewa kwenye kozi hiyo  ili kuona kama mtaala huo uko tayari na unajitosheleza  kuanza kutumika kwa walengwa kabla ya kozi rasmi ya wiki sita kuanza.
Mada zilizofundishwa ni; Basic ambulance safety, Documentation and Communications, Pre hospital trauma, Obstretics emergencies, Patient movement. Mwisho wa mafunzo hayo  wanafunzi walipewa  vyeti vya ushiriki wa mafunzo hayo

No comments :

Post a Comment