Katibu Tawala Msaidizi Sekta za
Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dodoma Bibi Aziza Mumbi akizungumza na
waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu faida za mfumo wa Kusajili
Kampuni kwa njia ya mtandao leo Jijini Dodoma.
Meneja Uboreshaji Mazingira ya
Biashara na Uwekezaji kutoka Baraza la Taifa la Biashara Bw. Willy
Magehema akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa
maafisa Biashara na TEHAMA wa Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma.
Sehemu ya Washiri wa Mafunzo hayo
wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya
mfumo wa Kusajili Kampuni kwa njia ya mtandao leo Jijini Dodoma
Katibu Tawala Msaidizi Sekta za
Uchumi na Uzalishaji Bibi Aziza Mumbi akiwa kwenye picha ya pamoja na
Washiri wa Mafunzo ya mfumo wa Kusajili Kampuni kwa njia ya mtandao leo
Jijini Dodoma.
Msajili Mwandamizi kutoka BRELA Bw. Lumambo Shiwala akisisitiza kuhusu umuhimu wa mfumo huo katika kukuza biashara.
( Picha zote na MAELEZO
………………
Na Mwandishi Wetu
Serikali imeanzisha Mfumo wa
Kielektroniki utakaotumika kusajili Makampuni, Majina ya Biashara,Leseni
za Viwanda, hati, Alama za biashara na huduma Kote nchini.
Akizungumza wakati akifungua
Mafunzo ya siku mbili kwa Maafisa Biashara wa Wilaya zote za Mkoa wa
Dodoma Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Dodoma anayeshughulikia Uchumi
na
Uzalishaji Bibi Aziza Mumba amesema kuwa mfumo huo utaongeza tija
kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wanaohitaji leseni za Biashara
kupitia mfumo huo wa kielektroniki.
Akizungumzia Mfumo huo Bibi Mumba
amesema umeanza kutumika kwa awamu ya kwanza kuanzia tarehe 4 Januari ,
2018 kwa kusajili alama za Biashara kwa njia ya mtandao ambapo mfumo
huo umeacha madirisha wazi kwa ajili ya kuweza kuunganisha na mifumo ya
Taasisi nyingine za Serikali zitakapokuwa tayari.
“Natoa shukrani za Dhati kwa mradi
wa uboreshaji mazingira ya Biashara kwa kuwezesha ujenzi wa vituo vya
biashara kwa Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma hali itakayowezesha
wafanyabiashara kupata huduma zote katika eneo moja” Alisisitiza Bibi
Mumba
Alifafanua kuwa kwa kuzingatia
umuhimu wa mfumo huo BRELA kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la
Biashara (TNBC) wameandaa mafunzo kwa watendaji wa vituo hivyo ili
kuwawezesha kutoa huduma kwa wafanyabiashara na wawekezaji watakaohitaji
msaada wa ziada katika kutumia mfumo huo katika kusajili makampuni kwa
njia ya mtandao.
Aliongeza kuwa washiriki wa
mafunzo hayo ambao ni Maafisa Biashar na Maafisa TEHAMA wana wajibu
wa kutoa elimu ya mfumo huo kwa wananchi wote kupitia Mabaraza ya
Madiwani ya Halmashauri na Mabaraza ya Maendeleo ya Kata.
Kwa upande wake Meneja Uboreshaji
Biashara na uwekezaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) amesema kuwa
ili kujisajili na kupata huduma zote katika mfumo huo wa TEHAMA lazima
mwombaji awe na kitambulisho cha Taifa.
Aliongeza kuwa mfumo huo utasaidia
kuongeza tija katika kusajili biashara na kusaidia urasimishaji wa
Biashara hali itakayochochea kukua kwa biashara hapa nchini.
Urasimishaji biashara ni hali
kuifanya biashara kutambulika kisheria kwa kuzingatia sheria, Kanuni na
taratibu zilizopo ambapo utoaji wa leseni za Biashara unasimamiwa na
sheria ya leseni za Biashara Na. 25 ya mwaka 1972 pamoja na marekebisho
yak echini ya sheria NA. 9 ya mwaka 1980.
Mfumo huu umeunganishwa na Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili ya namba za utambulisho wa
Taifa, Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya kutoa Namba ya
Utambulisho kwa mlipa kodi (TIN) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) kwa ajili ya utambuzi wa maeneo nchini.
No comments :
Post a Comment