Wednesday, April 18, 2018

WAZIRI WA NISHATI: NI MARUFUKU KURUKA NYUMBA WAKATI WA KUWAUNGANISHIA UMEME WA REA WANANCHI WEKENI HATA KWENYE NYUMBA ZA NYASI


1
Waziri wa  Dkt. Medard Kalemani (mwenye shati nyeusi) akitoa maelekezo jana wilayani Urambo baada ya kukagua njia ya kupeleka umeme vijiji unatekelezawa chini ya miradi inayosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijiji awamu ya Tatu.
2
Mbunge wa Jimbo la Urambo Magreth Sitta(kulia) akizungumza na wakazi wa kijiji cha Jioneemwenyewe Kata ya Songambele wakati wa sherehe za uwashaji wa umeme zilizozunduliwa na Waziri wa Nisha Dkt Medard Kalemani (hayupo katika picha) jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa.
3
  Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani) na Mbunge wa Urambo Magreth Sitta na viongozi wengine wakikata utepe wa uzinduzi wa uwashaji wa umeme wa REA katika Kijiji cha Jionee Mwenyewe kata ya Songambele jana.
4
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (mwenye miwani) akiwapungua mkono wananchi wa Kijiji cha Jionee Mwenyewe kata ya Songambele wakati wa sherehe za uwashaji umeme wa REA jana.
5
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akibonyesha kitufe kuwasha umeme katika Kijiji cha Jionee Mwenyewe Kata ya Songambele baada ya kukamilika kwa mradi wa uwekaji wa miundombinu katika eneo hilo.
6
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani) na Mbunge wa Urambo Magreth Sitta(kushoto) na wananchi wa kiijiji cha Jionee Mwenyewe kata ya Songambele wakishangilia mara baada ya uzinduzi wa uwashaji wa umeme katika eneo hilo jana.
7
Baadhi ya wanakijiji wa Jionee Mwenyewe Kata ya Songambele wakisikiliza Hotuba ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo katika picha ) mara baada ya kuzindua uwashaji wa umeme katika Kijiji chao jana.
8
  Waziri wa Nishati Medard Kalemani akimpongeza Diwani wa Kata ya Vumilia kupitia ACT Wazalendo Kassim Shushu (kushoto) baada ya kumkabidhi eneo la shamba lake linalokadiriwa
kuwa ekari moja kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Kupozea umeme.
Picha na Tiganya Vincent
RS Tabora
…………..
NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
SERIKALI imesema ni marufuku kwa Wakandarasi na Wataalamu kuruka nyumba wakati wa uunganishaji wa umeme kwa wananchi kupitia  Mradi kabambe wa kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatuunatekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA).
Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani Urambo na Kaliua na Waziri wa  Dkt. Medard Kalemani wakati alipokuwa akigaua utekelezaji wa zoezi la usambazaji wa umeme wa REA katika maeneo hayo.
Alisema ni marufuku kuruka nyumba hata kama ni nyasi kama mwananchi anataka umeme na amelipa shilingi 27,000 za kuunganishiwa umeme.
Kalemani alisema kuwa mpango wa Serikali ni kuhakikisha umeme unafika katika vijiji na vitongoji vyote na kwa wananchi wote bila kubagua.
“Nawaagiza Wakandarasi na Wataalamu wote hakuna kuruka nyumba wala kubagua nyumba kwa sababu ya kuwa imeezekwa kwa nyasi…umeme ni nyumba kwa nyuma , kaya kwa kaya.., hata kama mtu hajakamisha nyumba yake kama kuna mti karibu na nyumba yake wekeeni hata hapo ili iwe rahisi kuingiza umeme atakapokuwa amekamisha nyumba yake” alisisitiza Waziri huyo.
Alisisitiza kuna mtindo wa Wakandarasi kuchagua nyumba wakati wanapotekekeza majukumu yao ya kuwaweka umeme , na kusema kuwa kwa hivi sasa hilo ni marufku umeme ni kwa wote wanaotaka.
Waziri huyo wa Nishati aliongeza kuwa ni marufuku kuwatoza wananchi wanaotaka kuunganishiwa umeme zaidi ya shilingi 27,000/- na kutoa wito kwa mwananchi atayetozwa zaidi ya kiasi hicho atoe taarifa ili hatua kali dhidi ya wahusika ziweze kuchukiwa.
Aidha alitoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kuunganishiwa kwa gharama hizo kwani baada ya hapo itabidi walipie kulingana na taratibu za Shirilka la Ugavi wa umeme Tanzania(TANESCO)
Katika hatua  nyingine Waziri huyo wa Nishati amemupongeza Diwani wa Kata ya Vumilia Wilayani Urambo Kassim Shushu kwa kutoa eneo lake kwa ajili ya kuwapatia TANESCO ili wajenge kituo cha kupozea umeme.
Alisema kitendo hicho cha Diwani wa Kata ya Vumilia kupitia ACT Wazalendo ni cha kizalendo na kimeonyesha kuwa maendeleo hayana chama na baada ya kukamilisha mradi TANESCO itabidi waone jinsi ya kumpa mkono wa shukurani.
Dkt . Kalemani alisema  baada ya Shirika lake la la Ugavi wa Umeme Tanzania(TANESCO) litajenga Kituo kidogo cha kupozea umeme (sub station) katika Kijiji hicho cha Uhuru ili  kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wananchi wa Wilaya ya Kaliua na Urambo na maeneo jirani.
Alisema Kituo kikingine kitajengwa mpakani mwa Tabora na Kigoma kwa ajili ya kuuwezesha na Mkoa wa Kigoma kuwa na umeme wa uhakika.
Waziri huyo wa Nishati alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza tatizo la kukatika kwa umeme katika maeneo hayo.

No comments :

Post a Comment