Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi UNAMID
Jimboni Darfur Sudan Luteni Jenerali Leonard Ngondi ( wa Tatu kushoto)
akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Khor Abeche katika sherehe za
uvishaji nishani walinda Amani kutoka Tanzania Hivi karibuni wa nne
Kushoto ni kamanda wa kikosi cha Tanzania Kanali Wiliam Sandy .
Kamanda Kikosi cha Tanzania
TANZBATT 11 Jimboni Darfur nchini Sudan Kanali William Sandy kulia
akivishwa nishani na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi UNAMID Luteni Jenerali
Leonard Ngondi katika sherehe za uvishaji nishani walinda Amani kutoka
Tanzania Hivi karibuni.
Mnadhimu Mkuu wa mpango wa pamoja
wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID akivisha nishani walinda
Amani kutoka tanznaia katika sherehe za uvishaji nishani walinda Amani
kutoka Tanzania Hivi karibuni katika eneo la Khor Abeche
Picha na Luteni Selemani Semunyu.
………………
Askari wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania Kikosi cha 11 wametakiwa kujivunia mafanikio
yaliyopatikana kufuatia utumishi wao uliotukuka kwa kipindi cha Mwaka
Mmoja
waliokuwa wakishiriki Ulinzi wa amani Jimboni Darfur nchini Sudan
na kutunukiwa Nishani ya umoja wa Mataifa.
Hayo yalibainishwa na mkuu wa
majeshi ya Ulinzi ya umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID
jimboni Darfur Luteni Jenerali Leonard Ngondi wakati wa sherehe za
kuwatunuku Nishani Askari wa JWTZ katika sherrehe zilizofanyika Khor
Abeche na kuhudhuruliwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo wa Serkali ya
Sudan.
“ Kutunukiwa nishani ni jambo la
Kujivunia kwa kuwa zimetolewa kwa sababu Askari wamefanya kazi Nzuri
amabayo inapaswa kupongezwa hasa kutokana na Doria zilizofanyika ikiwemo
katika safu za Milima ya jaber ambayo inakaliwa na Waasi” Alisema
Luteni Jenerali Ngondi.
Kwa Upande wake Mkuu wa Operesheni
ya Jaber Mara Lameck Kawiche alitoa wito kwa Wanajeshi wa Tanzania
kuendeleza utayari wao ili kuhakikisha wanalinda heshima ya jeshi hilo
kwa kufanya kazi kwa Weledi ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea
kama ilivyotokea Nchini Kongo.
“ Najivunia Utimamu wa jeshi la
Tanzania tuna kila sababu kumpongeza Rais na Amiri Jeshi kwa kuridhia
Majeshi ya tanznia Kushiki Operesheni za Umoja wa Mataifa sambamba na
Mkuu wa Majeshi kya Ulinzi kwa mafunzo kwa Wanajeshi Wake” Alisema
Kawiche.
Pia Aliongeza Kuwa Wanjeshi katika
utendaji wao wa majukumu katika nchi yeyote ni kielelezo cha nchi
husika hivyo Nidhamu na Weledi wa Askari wa JWTZ ni kielelezo cha amani
na Fursa zilizopo katika nchi husika .
Kawiche aliwataka Wanajeshi wa
Tanzania kutumia Fursa ya kukubalika Kimataifa kuwa kivutio kwa Watalii
na wawekezaji lakini kutobweteka na sifa kwani maeneo ya Ulinzi wa amani
ni maeneo yanayoweka kubadilika wakati wowote.
Kamanda wa Kikosi hicho ambacho
kilifanikiwa kufika katika maeneo amabayo hayakuwahi kufikiwa na Umoja
wa Mataifa kmutokan na kukaliwa na waasi na Miundombinu mibovu Kanali
William Sandy aliahidi kuendeleza Nidhamu na kusema kauli za Viongozi
hai zimezidi kuwapa moyo wa kuafanya kazi kwa umakini ili kutoharibu
sifa ya jeshi na nchi kwa ujumla.
Nishani za Umoja wa mataifa kwa
Askari polisi na Wanajeshi Walinda Amani zilianza kutolewa mwaka 1950 na
kwa Sudan Jimboni Darfur zilianza kutolewa Mwaka 2008.
No comments :
Post a Comment