
Kiongozi wa mbio za mwenge,Charles
Kabeho akifungua bomba kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji wa Kasanda
iliofadhiliwa na Water Mission Tanzania.
Shamrashamra za uzinduzi wa mradi
Kiongozi wa mbio za mwenge,
Charles Kabeho, akiongea na wananchi wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji
Kasanda,(kushoto) ni Mkurugenzi wa Kanda wa shirika la kimataifa la
Water Mission, Will Furlong
Shirika la kimataifa la Water Mission Tanzania lafanikisha mradi wa maji safi na salama katika Kijiji cha Kasanda
Wakazi wa kata ya Kasanda,
wilayani Kakonko mkoani Kigoma, jana,wameanza kupata maji
safi na salama
kutokana na kuzinduliwa kwa mradi mpya wa maji chini ya ufadhili wa
Shirika la kimataifa la Water Mission Tanzania. Mradi huu utanufaisha
zaidi ya kaya 729 zinazoishi maeneo hayo.
Miradi ya Kakonko na Kasanda, ni
miongoni mwa miradi zaidi ya 20 ya kuwapatia wananchi maji safi na
salama ambayo imetekelezwa na shirika la Water Mission Tanzania tangu
mwaka 2014. Miradi ya Kasanda na Kakonko ni tofauti na ile
iliyotekelezwa maeneo mengine kwa kuwa iko katika maeneo yaliyopo karibu
na kambi ya wakimbizi ya Mtendeli.
Mkurugenzi wa Kanda wa shirika la
kimataifa la Water Mission, Will Furlong alisema “Water Mission
Tanzania, kupitia ufadhili wa taasisi ya Poul Due Jensen Foundation
ambayo zaidi inajulikana kama, Grundfos Foundation, imewezesha
ufanikishaji miradi 8 ya maji safi na salama kwa jamii mbalimbali
nchini. Mradi mwingine wa Zeze mkoani Kigoma nao tayari umezinduliwa
mwezi huu. Mashirika ya Water Mission Tanzania na Grundfos Foundation,
yanashirikiana kuhakikisha huduma za maji safi na salama zinafikia jamii
zenye changamoto katika kanda ya Afrika Mashariki”.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa
mradi huu mkubwa wa maji ulioambatana na sherehe za mbio za Mwenge
katika kata hiyo,Kiongozi wa mbio za mwenge,Charles Kabeho,alisema kuwa
kuzinduliwa kwa mradi huo ni jambo la kihistoria kwa wakazi wa eneo hilo
ambalo kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kupata
maji safi na salama.
“Kwa niaba ya serikali napenda
kutoa shukrani kwa wadau wa maendeleo wanaounga mkono jitihada za
serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazokabili jamii
kama ambavyo hawa wenzetu wa Water Mission Tanzania ,wamekuwa mstari wa
mbele kufanikisha miradi ya maji sehemu mbalimbali hapa nchini”alisema
Kabeho.
Alisema kero ya ukosefu wa maji
safi na salama kwa muda mrefu ilisababisha akina mama kutembea mwendo
mrefu kutafuta maji sambamba na wananchi wengi kuathirika kwa kupata
magonjwa mbalimbali kutokana na kutumia maji yasio salama kwa matumizi
ya binadamu.
Kabeho,alitoa wito kwa wakazi wote
wa eneo hilo kujiona ni sehemu ya mradi huu na kuhakikisha wanatunza
miundo mbinu ya mradi wakati wote sambamba na kutoa ushirikiano kwa
wataalamu wanaofanya ushauri wa uendeshaji mradi.


No comments :
Post a Comment