00:00
01:17
01:17
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye mkutano
wa Jukwaa la Wanawake ikiwa Sehemu ya mkutano wa Jumuiya ya Madola
unaofanyika jijini London, Uingereza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia na Waziri Mkuu
wa Malta Mhe. Dkt. Joseph Muscat mara baada ya mkutano wa Jukwaa la
Wanawake kumalizika jijini London, Uingereza.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
………………..
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan, jana jioni alikuwa
ni miongoni mwa Jopo lililojadili kuhusu sera za kumwinua mwanamke
kiuchumi wakati wa mkutano wa Jukwaa la Wanawake linalofanyika kama
sehemu ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola
(CHOGM) unaoendelea hapa London.
Kwenye jopo hilo Mheshimiwa Makamu wa Rais aliungana na Mhe.
Dkt. Joseph Muscat, Waziri Mkuu wa Malta na wadau wengine wa masuala ya
maendeleo ya wanawake.
Makamu wa
Rais aliweza kuelezea hatua mbalimbali ambazo serikali kali imechukua
ili kumwinua mwanamke kiuchumi ikiwa pamoja na kuwapatia haki ya
kumiliki ardhi, kuboresha elimu kwa mtoto wa kike, kuwapa nafasi za
uongozi na pia Serikali ipo kwenye hatua za kuhakikisha mikopo yenye
riba nafuu kwa Wanawake.
Makamu wa Rais yupo jijini London kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola.
No comments :
Post a Comment