
Mkurugenzi
wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa
akionyesha vipeperushi vya kampeni mpya ya Benki hiyo kwa wateja wake,
ijulikanayo kama #TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiajiwa kadi za
malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda
kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia, zitakazofanyika nchini
Urusi kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Mkurugenzi
wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akitangaza kampeni
mpya ya Benki hiyo kwa wateja wake, ijulikanayo kama #TwenzetuRussia,
itakayowawezesha watumiajiwa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki
hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe
la Dunia, zitakazofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Benki
ya CRDB leo imetangaza kuanza rasmi kwa kampeni ijulikanayo kama
“Furahia kandanda murua nchini Urusi” #TwenzetuRussia, itakayowawezesha
watumiaji wa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia
safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia
zitakazofanyika nchini Urusi, kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo,
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo Bi.
Tully Esther Mwambapa, alisema kuwa Benki ya CRDB imeanzisha kampeni kwa
kushirikiana na kampuni ya Visa International ili kutoa fursa kwa
wateja wake kwenda kushuhudia fainali hizo, ambazo huvutia hisia za watu
wengi dunuani kote.
“Wateja
wetu wenye TemboCardVisa, TemboCardVisa-Electron, TemboCard Visa-Gold,
TemboCardVisa- Platinum na TemboCardVisa-Infinite, wakati wa kampeni hii
watatakiwa kulipia bidhaa au huduma wanazonunua kwa kutumia
TemboCardVisa zao kupitia mashine za malipo (POS) zilizopo sehemu
mbalimbali kama kwenye migahawa, maduka, mahospitali, vituo vya mafuta
na kwingineko, ili waweze kujishindia zawadi hii kubwa” alisema.
Bi.Mwambapa
aliendelea kusema kuwa “iii mteja aweze kushinda, anatakiwa kufanya
miamala mingi zaidi kila wiki na kadri mteja anavyolipia zaidi kwa
kutumia TemboCardVisa yake, ndivyo anavyojiongezea nafasi kubwa zaidi ya
kushinda.
Washindi
wa wawili watakaokuwa wamefanya miamala mingi zaidi kila wiki
watajishindia safari ya kwenda Urusi ambayo itagharamiwa kila kitu na
Benki ya CRDB, ambapo jumla ya tiketi 24 zitatolewa” alisema Bi. Tully
Mwambapa.
Bi.Mwambapa
aliendelea kusema kuwa pamoja na washindi wawili wa kwanza kujishindia
safari hiyo, Benki pia kila wiki itatangaza washindi wengine 10 kupitia
vyombo mbalimbali vya habari ambao watajishindia zawadi kemkem ikiwemo
luninga zitakazokuwa zimeunganishwa na kulipiwa kinga’muzi cha DSTV,
jezi za timu za mataifa mbalimbali, mipira, kofia, fulana na na zawadi
zingine nyingi.

No comments :
Post a Comment