Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya
Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimzibua mgonjwa
mishipa ya damu ya moyo ambayo imeziba kwa kutumia mtambo wa Cathlab
katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa
kutumia tundu dogo inayofanyika katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa
23 wamezibuliwa mishipa ya damu pamoja na kufanyiwa uchunguzi.
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya
Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Taasisi ya
Madaktari Afrika ya nchini Marekani wakimzibua mgonjwa mishipa ya damu
ya moyo ambayo imeziba kwa kutumia mtambo wa Cathlab katika kambi maalum
ya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa kutumia tundu dogo
inayofanyika katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 23 wamezibuliwa
mishipa ya damu pamoja na kufanyiwa uchunguzi.
Picha na Brighton James – JKCI
……………..
Brighton James – JKCI
27/4/2018 Watanzania wameshauriwa
kufanya mazoezi, kula vyakula bora, kuepuka uvutaji wa sigara na unywaji
wa pombe uliokithiri kwa kufanya hivyo watajiepusha na magonjwa ya
mishipa ya damu ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yanaouwa watu wengi
Duniani.
Ushauri huo umetolewa leo na
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya
Madaktari Afrika ya
nchini Marekani Mazen Albaghded wakati akiongea na waandishi wa habari
katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa
kutumia tundu dogo inayofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI).
Dkt. Albaghded alisema kuwa ulaji
wa vyakula vyenye mafuta na bila kufanya mazoezi ambayo yangesaidia
kuyeyusha mafuta hayo kunaweza kusababisha kupata kirahisi ugonjwa wa
mishipa ya damu ya moyo. Wagonjwa wa kisukari na wenye shinikizo la juu
la damu nao wanaweza kupata ugonjwa huo kirahisi.
“Mishipa ya damu inapozungukwa na
mafuta baadaye huweza kuziba na hivyo damu kushindwa kwenda katika
misuli ya moyo (myocardium) na kusababisha mtu kupata shambulio la
moyo”, alisema.
Akizungumzia kuhusu kambi hiyo ya
matibabu ya siku nne Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete Tulizo Shemu alisema wagonjwa wanaotibiwa ni wale wanaohitaji matibabu ya kibingwa yenye uhitaji wa uchunguzi yakinifu.
Dkt. Shemu alisema kwa kutumia
mtambo wa Cathlab kwa njia ya kutoboa tundu dogo kwa mgonjwa wanaangalia
kama mishipa ya moyo imeziba na ikiwa imeziba wanaizibua kwa kumuwekea
mgonjwa kifaa maalum kinachojulikana kwa jina la “stent” ambacho
kinasaidia mshipa wa damu usizibe tena.
Katika kambi hiyo ambayo ilienda
sambamba na mafunzo ya kubadilishana ujuzi wa kazi jumla ya wagonjwa 23
wamefanyiwa vipimo na matibabu ambapo hali zao zinaendelea vizuri na
wengine wameruhusiwa kurudi nyumbani.
No comments :
Post a Comment