Basi lililokuwa limebeba askari
Polisi limegongana na gari dogo aina ya Noah iliyokuwa imebeba Wanajeshi
wa JWTZ, katika maeneo ya Bwawani mkoani Morogoro.
Imeelezwa kuwa basi hilo la Polisi
lilikuwa likitokea jijini Dodoma kwenye sherehe za Muungano
zilizofanyika jana Aprili 26, 2018 huku Noah hiyo iliyokuwa na Wanajeshi
takribani 6 pamoja na mtoto ikitokea Morogoro. Majeruhi wote
wamepelekwa hospitali Morogoro
Hata hivyo, bado hakuna taarifa
rasmi lakini habari za awali zinasema askari wawili wamefariki papohapo
ingawa Kamanda wa Polisi, Ulrich Matei amesema atatoa taarifa za kina
baaadae.
No comments :
Post a Comment