Mwakilishi Taasisi ya
Twaweza Bi. Anastazia Rugaba akitoa maoni mara baada ya kumalizika kwa mjadala
kwenye makundi uliolenga kutoa maoni juu ya uboreshaji wa Sera ya Taifa ya
Mashirika Yasiyo ya kiserikali wakati wa kikao kazi kilichofanyika
Jijini Arusha.
NA MWANDISHI WETU- ARUSHA
SERIKALI imeagiza
Mashirka yote Yasiyo ya Kiserikali kuhakikisha wanajihakiki katika Ofisi ya
Msajili wa Mashirika hayo iliyopo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto na ifikapo mwezi Mei mwaka huu na zoezi hilo
litasitishwa rasmi.
Hayo yamesemwa leo
Jijini Arusha na Msajili wa Mashirka Yasiyo ya kiserikali nchini Bw. Marcel
Katemba alipokuwa akifunga kikao kazi cha wadau wa NGOs nchini kilichokuwa
kinajadili kuhusu maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Bw. Katemba amesema
kuwa zoezi hili limechukua muda mrefu sana na wamekuwa wakiongeza muda mara kwa
mara ili kuyapa nafasi mashirika ambayo hayakujihakiki kufanya hivyo.
Ameongeza kuwa mara
baada ya kumalizika kwa zoezi hilo mwezi Mei mwaka huu wataweka majina ya
Mashirika yote ambayo yatakuwa yamejihakiki kwenye Tovuti mpya ya Msajili na
yale yote ambayo yatakuwa hayajajihakiki hayataruhusiwa kufanya kazi nchini.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Bw. Nicholous
Zakaria ameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa NGOs kwa ushirkiano
wanaowapa kama Baraza na kwa wadau wote wa NGOs nchini.
Mwakilishi Shirika la
TAVICO Bw. Charles Nkwabi akitoa maoni mara baada ya kumalizika kwa mjadala
kwenye makundi uliolenga kutoa maoni juu ya uboreshaji wa Sera ya Taifa ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati wa kikao kazi kilichofanyika
Jijini Arusha.
Msajili wa Mshirika
Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba akitoa neno kwa wadau wa Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi
kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya
Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Mkurugenzi Msaidizi Usajili NGOs Bw. Leornald Baraka akichangia jambo
katika mjadala wa wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali uliojikita kujadili
maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati wa
kuhitimishwa kwa kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha
Baadhi ya wadau wa Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali wakiwa katika makundi wakijadili na kutoa maoni kuhusu
maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao kazi
kilichofanyika Jijini Arusha.
Baadhi ya wadau wa Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali wakiwa katika makundi wakijadili na kutoa maoni kuhusu
maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao kazi
kilichofanyika Jijini Arusha. (PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO WAMJW)
No comments :
Post a Comment