Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.
Evod Mmanda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara akipokea vitabu kutoka
kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Profesa
Benadeta Kiliani .
Vitabu hivyo vya Kiada kwa darasa la 1-4 vinasambazwa na TET kwa kwa mikoa yote Tanzania na leo ilikuwa zamu ya Mtwara.
Hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu hivyo imefanyika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara.
Katika hotuba fupi aliyoitoa Mhe.
Mmanda wakati wa mapokezi hayo amesema anaridhishwa na jitihada za
serikali ya awam ya tano katika kuinua elimu ya Tanzania.
Kwa upande wake Profesa Benadeta
Kiliani amezitaka Halmashauri zote zilizokwisha pokea vitabu hivyo
zihakikishe zinavifikisha kwa walengwa ambao ni wanafunzi.
No comments :
Post a Comment