JAJI mkuu wa Zanzibar Omar
Othman Makungu, amewauliza mahakimukisiwani Pemba, wamezitoa wapi sheria
zinazowapa mamlaka yakuwalazimisha watuhumiwa kuwa na wafanyakazi wa
serikali au barua zamasheha wanapoomba dhamana dhidi ya kesi
zinazowakabili.
Alisema anashangaa
kuona baadhi ya mahakimu hao, kuwawekea mashartimagumu watuhumiwa, kwa
lengo la kutafuta sababu ya kuwapelekearumande, jambo ambalo sio sahihi
maana huko sio kwahali kwema kwakukaa mwanadamu.
Jaji Mkuu huyo
alieleza hayo kwa nyakati tofauti, walipokuwaakizungumza na watendaji wa
mahakama za mwanzo Wingwi, Konde na Wete,ikiwa ni sehemu ya ziara yake
ya siku nne kisiwani kisiwani Pemba.
Alisema lazima
mahakimu wafahamu kuwa, kumpeleka mtuhumiwa rumande nihatua ya mwisho,
na sio iwe ndio kipaumbele chao, kwa kuwekea mashartimagumu au kima
kikubwa cha fedha.
Alieleza kuwa, yeye
binafsi hajaona popote kwenye sheria, kuwamtuhumiwa anatakiwa ili
kutimiza masharti kwamba awe na mtuanaefanyakazi serikalini, au barua ya
sheha kwamba ndio kigezo namtuhumiwa akishindwa na hayo, apelekwe
rumade.
“Jamani wale ni
binadamu, wapo waliotenda makosa, wapo walioteleza nawengine
wamesingiziwa sasa na nyinyi mkishawishika kwa kuwapelekarumade, tena
kwa masharti mazgumu, mtakuwa hamkuwatendea haki’’alieleza.
Katika hatua nyengine
Jaji Mkuu huyo wa Zanzibar alisema, mahakimulazima wafanye kazi
kisayansi na sio kufanya kazi kwa mashindikizo yawanasiasa, maana
wakifanya hivyo watakuwa hawaitendei haki fani yao.
“Lazima muelewa
mahakimu wetu kwamba, kuna kupanda daraja kwa mujibuwa kazi zenu, lakini
kama mnafanyakazia kwa chuki, mashindikizo basimsitarajie kupanda
ngazi,”alieleza.
Nae Mrajis wa Mahakama
kuu Zanzibar Mohamed Ali Mohamed, alisema sasawatakuwa na makini na
mahakimu watoro na wanaopenda kusafiri bila yadharura maalum.
“Wapo mahakimu
unawaona Unguja mara kwa mara bila ya safari maalum zakikazi, na huku
wameziacha kesi juu ya meza na kuwatia watu tabu, sasahawa tutapambana
nao,”alieleza.
Nae Mrajisi wa jimbo
mahakama kuu Pemba Hussein Makame Hussein,alisema changamoto kadhaa
wamezisikia hawa walipowatembelea wanafunzi,juu ya kucheleweshea
mienendo ya kesi, jambo kwa sasa wanajitahidi.
Ziara ya Jaji Mkuu Zanzibar akiwa na Mrajisi na
Manaibu Warajisi,itaendelea tena kesho kwa kulikagua jengo la Mahakama
Kuu Chakechakekabla ya kuzungumza na watendaji wake, na kukamilisha
ziara yake ya siku nne kisiwani Pemba .
No comments :
Post a Comment