Monday, April 23, 2018

COCA-COLA BONITE YAMWAGA ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA ‘MZUKA WA SOKA NA COKA’


 Mmoja wa washindi wa pokipiki akikabidhiwa zawadi yake.
Baadhi ya washindi wa luninga katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa zawadi zao
Washindi wa pikipiki wakijaribu kuendesha pikipiki zao baada ya kukabidhiwa wakiwa na Meneja Mauzo wa Bonite, Boniface Mwassi.
Wshindi wa fedha taslimu shilingi 100,000/-baada ya kukaidhiwa zawadi zao na Afisa Mwandamizi wa Mauzo wa Bonite, Godfrey Imani.
Baadhi ya washindi wakisubiri kukabidhiwa zawadi zao
Wakazi 25 wa miji ya Moshi na Arusha wameimaliza wiki kwa furaha baada ya kukabidhiwa zawadi zao walizojishindia kupitia promosheni ya kiwanda cha Coca-Cola cha Bonite kilichopo mjini Moshi inayojulikana kama “Mzuka wa Soka na Coka”Zawadi walizojishindia wananchi hao ni pamoja na
pikipiki 3,televisheni 7,na 15 pesa taslimu shilingi 100,000/-
Akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi hizo,Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Bonite Bottlers, Chris Loiruk,alisema kampuni inayo furaha kuona wateja wake wataendelea kushiriki katika promosheni hii na kuweza kujishindia zawadi mbalimbali.
Alisema Promosheni hii iliyozinduliwa mapema mwezi huu itanufaisha watumiaji wa vinywaji vinavyotengenezwa na kampuni ya Coca-Cola ambavyo ni Coca-Cola, Sprite, Fanta, Sparletta, Schweppes Stoney Tangawizi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida .”Zipo zawadi nyingi zimeandaliwa kwa ajili ya wateja wetu zikiwemo pikipiki,luninga bapa za kisasa,fedha taslimu kuanzia 5000 hadi 100,000/-na soda za bure, tunatoa wito waendelee kushiriki waweze kujishindia”.Alisisitiza Loiruk.
Wakiongea kwa furaha baada ya kukabidhiwa zawadi zao washindi hao waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kuandaa promosheni zenye mwelekeo wa kuwakwamua wateja wake kimaisha sambamba na kuleta furaha kwa familia kupitia kuangalia luninga za kisasa.
Akiongea kwa niaba ya washindi wa pikipiki, Elisha Nanyaro Mkazi wa Tengeru, mkoani Arusha,alisema kuwa wanayo furaha kubwa kwa zawadi waliyojishindia na chombo hicho kinasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha usafiri sambamba na matumizi ya biashara kwa ajili ya kuongeza pato la familia.
Naye mmoja wa washindi Fransisca Mtuy,akiongea kwa niaba ya washindi wa luninga,alisema kuwa ushindi wa zawadi zao umekuja kwa wakati mwafaka ambapo mashindano ya soka ya kombe la Dunia yanakaribia,hivyo wataweza kuyaangalia pamoja na familia zao kwa kutumia luninga nzuri pia wataweza kufurahia habari na vipindi mbalimbali .
Kwa upande wake,Hawa Abrahamani,mjasiriamali na mkazi wa Arusha, akiongea kwa niaba ya washindi wa fedha taslimu shilingi 100,000/-alisema kuwa fedha walizojishindia zitawawezesha kutatua matatizo mbalimbali yaliyokuwa yakiwakabili sambamba na kuongeza mitaji yao ya biashara

No comments :

Post a Comment