Mkuu wa mkoa wa Songwe, Luteni
Mstaafu, Chiku Galawa akiteta jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora wakati wa ziara ya
kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa maboresho ya Mazingira ya
biashara na uwekezaji mkoani Songwe, tarehe 17 Machi, 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora akiendesha kikao kilicho
jumuisha watendaji wa serikali na sekta binafsi wakati wa ziara ya
kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa maboresho ya Mazingira ya
biashara na uwekezaji mkoani Songwe, tarehe 17 Machi, 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora akiongozwa na Meneja wa
Kituo cha Forodha cha Pamoja Tunduma, Jomimosa Nsindo wakati wa ziara ya
kutembelea maeneo ya utekelezaji wa maboresho ya Mazingira ya biashara
na uwekezaji , mpakani mwa Tanzania na Zambia, tarehe 17 Machi, 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora akifuatilia maelezo ya
wateja wa Kituo cha Forodha cha Pamoja Tunduma (hawapo pichani) wakati
wa ziara ya kutembelea maeneo ya utekelezaji wa maboresho ya Mazingira
ya biashara na uwekezaji , mpakani mwa Tanzania na Zambia, tarehe 17
Machi, 2018.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
…………….
Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya
Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini, imeamua
kuzikutanisha wizara saba zinazohusika moja kwa moja na changamoto
zinazopunguza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara na
Wawekezaji
mpakani mwa Tanzania na Zambia.
Akiongea wakati wa ziara ya
kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa maboresho ya Mazingira ya
biashara na uwekezaji katika mkoa wa Songwe na maeneo yaliyopo mpakani
mwa Tanzania na Zambia, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na
Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora amesema mara baada ya kuhitimisha
ziara yake tarehe 17 Machi, 2018, atakutana na makatibu wakuu wa wizara
zinazopaswa kutoa suluhisho la changamoto hizo.
“Nitakutana na makatibu wakuu
wenzangu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara
ya Mambo ya nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za mikoa na Serikali za mitaa
(TAMISEMI) na naamini maazimio tutakayotoa katika kikao hicho yatakuwa
suluhisho la kuondoa changamoto zinazojitokeza hapa mpakani mwa Tanzania
na Zambia” , amesema Kamuzora.
Akibainisha changamoto za
mazingira ya Biashara na uwekezaji mpakani mwa Tanzania na Zambia, Mkuu
wa mkoa wa Songwe, Luteni Mstaafu, Chiku Galawa amesema, changamoto
kubwa mpakani hapo ni usalama kwa wafanyabiashara na biashara zao,
ambapo kwa mazingira ya mpaka huo imekuwa vigumu kuuimarisha.
“Mpaka wetu umejengwa kila
mahali , hivyo uhalifu unakuwa mgumu kuuzuia Kuna watu wanakunywa pombe
Zambia ambazo tumezizuia hapa nchini kuuzwa, na kurudi wamelewa Tunduma,
suala la biashara haramu ya ubadilishaji wa fedha inayofanywa mtaani
kinyume na sheria na taratibu za nchi ni changamoto , lakini
wafanyabiashara wanakwepa kodi kutokana na kuwa kunabaadhi ya watanzania
sehemu ya nyumba zao zipo Zambia nyingine ipo Tanzania hivyo ushuru wa
forodha haukusanywi kwa madai wanapeleka bidhaa hizo kwa watanzania
kwani hawapitishi bidhaa hizokwenye lango husika” alisema Galawa
Galawa amebainisha mipango ambayo
Mkoa umejipanga katika kuhakikisha wanakabili changamoto hizo, kuwa ni
kuliweka Daftari la wakaazi katika mfumo wa kielektroniki ambalo
litajumuisha wakaazi wote wa Tunduma kuanzia umri wa mwezi mmoja na
litakuwa linahuishwa kila wakati, Upimaji wa mji waTunduma nao
unaendelea na kila mmiliki wa ardhi atapewa hati, pia litajengwa soko
kubwa mpakani hapo ili kufanya menejimenti ya biashara mpakani.
Aidha, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu alikutana na wadau wa sekta binafsi, pamoja na wateja katika Kituo
cha Forodha cha Pamoja Tunduma, ambao walishauri sekta zinazohusika na
Mazingira ya Biashara na Uwekezaji mpakani hapo kwa upande wa Tanzania
na Zambia zikutane ili kuharakisha kutatua changamoto zinazopunguza
ufanisi wa biashara mpakani hapo.
Lengo la Mpango wa Kuboresha
Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini ni Kupunguza gharama za
Kufanya biashara nchini kwa kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa
wafanyabiashara na Wawekezaji, mpango huo unaotekelezwa na Idara,
Wizara na Wakala wa Serikali kwa uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
No comments :
Post a Comment