Mwenyekiti wa
muungano wa akinamama wa mkoani Pwani ,(Pwani Generation Queens ),Betty
Msimbe akizungumza wakati walipotembelea kituo cha kulelea watoto yatima
cha Buloma kilichopo kata ya Sofu,Pichandege wilayani Kibaha
Mwenyekiti wa
muungano wa akinamama wa mkoani Pwani ,(Pwani Generation Queens ),Betty
Msimbe (wa kushoto ) akimkabidhi vyakula na vifaa mbalimbali matron wa
kituo cha Buloma , Simpho Aidan(wa kulia)
Watoto wanaolelewa
kituo cha kulelea watoto cha Buloma foundation kilichopo kata ya Sofu
,Pichandege Kibaha wakionyesha vifaa walivyopokea kutoka kwa kikundi cha
Pwani Generation Queens ),wakati walipokwenda kuwatembelea na kutoa
misaada mbalimbali Sofu.
Picha na Mwamvua Mwinyi
………………
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
WAZAZI na walezi wameaswa kuacha tabia ya
kuwakatisha masomo watoto wao wa kike kwa makusudi ya kuwageuza kitega
uchumi kwa kuwaoza kwa vibopa na badala yake wawape haki yao ya elimu .
Aidha jamii imetakiwa
kujenga tabia ya kuwawezesha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu,
yatima na vituo vinavyosaidia watoto hao ikiwa ni pamoja na kuwapa
mahitaji muhimu hasa elimu, mavazi na malazi.
Rai hiyo ilitolewa na
mwenyekiti wa muungano wa akinamama wa mkoani Pwani ,(Pwani Generation
Queens ),Betty Msimbe wakati walipotembelea kituo cha kulelea watoto
yatima cha Buloma kilichopo kata ya Sofu,Pichandege wilayani Kibaha.
Betty alieleza wakiwa
ni wazazi na wanawake wameona watembelee watoto waliopo kituoni hapo na
kuwapatia msaada wa mchele kilo 100,mafuta ya kupikia,sabuni za maji
,sabuni za kufulia ,peds ,sabuni za kuoga,unga,sukari,mafuta ya kupika
na vifaa mbalimbali .
Alisema vituo hivyo
ni msaada mkubwa ambapo husaidia kuishi na watoto waliotelekezwa kwa
makusudi,wazazi kutengana ,kutupwa wakiwa wadogo na wengine kukimbia kwa
wazazi baada ya kutaka kulazimishwa ndoa za utotoni .
“Sisi kama wazazi
tumejitoa kwa kidogo chetu ,naomba wadau wa maendeleo na wenye uwezo wa
kifedha ,watembelee vituo na kutoa misaada kwa watoto hawa kwa
kushirikiana na serikali pia” alisema Betty.
Hata hivyo
,alisikitishwa kuona kuna msichana ambae alifikishwa kituoni hapo
kupitia ustawi wa jamii kutokana na mzazi wake wa kiume kutaka
kumkatisha masomo ili amuoze.
“Wazazi tuache tamaa
,yaani unamuachisha mtoto wako shule kisa umfanye mtaji ,upate fedha
,tuwasomeshe watoto wetu wa kike kwani nao ni sawa na wale wa kiume”
“Tusiwabague watoto kwa jinsia zao ,kila mmmoja ana haki ya kupata elimu ‘” alisisitiza Betty.
Akizungumzia kuhusu
muungano huo ,alifafanua kuwa wapo kikatiba wana wanachama 75 ,wana
akaunti na fedha ya akiba sh. mil .Tisa ,wanaendelea na miradi midogo
ambapo wanatarajia kusheherekea mwaka mmoja wa umoja wao ifikapo april 8
mwaka huu.
Makamu Mwenyekiti wa
Pwani generation queens , Elizabeth Ngai ,alisema kutoa ni moyo na sio
utajiri,hivyo jamii iwatupie jicho watoto yatima ili wafikie ndoto zao.
Alisema watoto hao
wengi wao wamefikia hapo kutokana na matatizo ya wazazi na walezi wao na
hawakukusudia kuishi maisha waliyonayo.
Nae mtoto anaelelewa
katika kituo hicho Neema Madei ,alisema baba yake alimkatisha masomo
akiwa na miaka 12 ili amuozeshe kwa mtu kama babu yake .
Alielezea ,mama yake
alikuwa nae pamoja ambapo alifikisha taarifa hiyo ustawi wa jamii ambao
walimpeleka kituo cha Buloma foundation na sasa yupo darasa la tano .
“Nawashukuru ustawi
wa jamii kwa kufungua maisha yangu kwakuwa sikutaka kuolewa ,na nawaasa
wazazi wenye tamaa waache tamaa zao na wawasomeshe watoto wao wakike
,wasikimbilie fedha waangalie haki za watoto” alisisitiza Neema.
Kwa upande wake
,matron wa kituo cha Buloma , Simpho Aidan ,alisema wanakabiliwa na
changamoto ya ukosefu wa uzio ,bima ya afya kwa ajili ya watoto hao na
jengo la watoto wakiume.
Aliwaomba wadau wenye uwezo wawaunge mkono ili kuondoa changamoto hizo.
Simpho alisema ,kituo
hicho kinawalea watoto 38 ,na wapo ambao wamefika kidato cha tano na
sita na wengine wanasoma chuo cha ufundi (VETA).
No comments :
Post a Comment