Wakazi wa kata ya Nshambia wakiwa
katika foleni ya kusubiri kupigwa picha wakati wa zoezi la Usajili
Vitambulisho vya Taifa; pamoja na mvua kubwa zilizokuwa zikiendelea
kunyesha.
Pichani ni Afisa uhamiaji Bw. Issa
Juma akifanya mahojiano na Bi. Kemilembe Ishengoma wakati wa zoezi la
uandikishaji Vitambulishi vya Taifa kwa wakazi wa Manispaa ya Bukoba
Mjini.
Pichani ni Bi. Hadija Abeid, Afisa
Usajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akitoa maelekezo kwa wananchi
wa kata ya Nshambya waliojitokeza kusajiliwa wakati wa zoezi la
uandikishaji Vitambulisho vya Taifa.
Pichani ni Bw. Daniel Michael
Afisa Usajil akimsaidia Bi. Monica Kagasheki kukamilisha zoezi la
uchukuaji alama za vidole wakati wa Usajili wa Vitambulisho vya Taifa.
Baadhi ya wakazi wa kata ya
Nshambya wakisubiri kukamilisha usajili wa Vitambulisho vya Taifa wakati
zoezi hilo likifanyika katika kituo cha Chuo kikuu Huria kata ya
Nshambya Manispaa ya Bukoba.
…………………
Wananchi mkoani Kagera wameeleza
kero kubwa wanayoipata, ukiwemo usumbufu mkubwa wanapokuwa kwenye
shughuli zao nje ya mkoa hasa maeneo ya mpakani kwa kukosa Vitambulisho
vya Uraia.
Hayo wameeleza wakiwa kwenye vituo vya Usajili unaoendelea mkoani humo; ukihusisha
Wilaya zote za Mkoa Kagera.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
wananchi hao wamedai kuwa lengo la kujitokeza kwa wingi ni kutokana na
umuhimu wa Vitambulisho hivi; kwani wengi wao hupata shida pindi
wanapotoka nje ya mkoa wao ikizingatiwa kuwa mkoa huo upo pembezoni
kabisa mwa nchi ya Tanzania.
Wakazi wa kata ya Nshambya Wilaya
ya Bukoba ni miongoni mwa wananchi waliojitokeza licha ya changamoto ya
mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Akizungumzia zoezi hilo; Kaimu mtendaji kata ya Nshambya
Bi Fatma Christian Majengo, amesema wananchi waliojitokeza ni wengi na
kuwataka wananchi wa eneo hilo kutokubali kuuziwa fomu za Vitambulisho
vya Taifa, kwani fomu hizo zinatolewa.
Kwasasa zoezi hilo limekuwa
linaendeshwa kwa Kata ili kutoa fursa kwa kila mwananchi kupata fursa ya
kusajiliwa; hivyo wananchi wametakiwa kuwa makini kufuatilia ratiba ya
lini zoezi litafika kwenye Kata zao.
No comments :
Post a Comment