Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isac Kamwelwe (Mb) akiongea na watendaji wa
wizara, pamoja na taasisi zake (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika
ofisini kwake Dodoma leo. Waziri Kamwelwe katika kikao hicho amesisitiza
kufanya kazi kwa ubora, ndani ya muda mfupi
na kutoa huduma kwa wananchi ndio jambo la msingi.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akitoa neno la
utangulizi katika kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wa wizara na taasisi
zake leo. Prof. Mkumbo amesisitiza utoaji wa huduma na utekelezaji wa miradi
mbalimbali inayowalenga wananchi wa Tanzania ni picha inayojieleza kuwa
serikali ipo na wananchi ndio namba moja katika huduma hizo.
Sehemu
ya watendaji waliohuduhuria kikao hicho wakimsikiliza Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhandisi Isac Kamwelwe (Mb), hayupo pichani.


No comments :
Post a Comment