Dar es Salaam, 19 Machi, 2018. Kampuni
inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania imeingia
katika makubaliano ya kipekee na kampuni ya kiteknologia ya Uber.
Kuanzia leo, wateja wote wa Tigo watatumia huduma za Uber App bure!
Makubaliano haya ya aina yake yatawafaidi watumiaji wa huduma za usafiri
za Uber pamoja na madereva waliojiunga na mfumo huo.
“Tigo
ni nembo pana ya biashara katika soko la Tanzania na tuna wajibu wa
kuzindua njia bora zaidi kwa wateja kujumuika katika maisha
yanayowazingira. Makubaliano haya na Uber yanaboresha bidhaa na huduma
ambazo wateja wetu wanafurahia katika maisha yao ya kila siku,”
Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema.
Naye
Alfred Msemo, Mkurugenzi wa Uber alisema, “Tunafurahia makubaliano haya
na Tigo yatakayowawezesha watumiaji na madereva wa huduma za Uber
waliojisajili na mtandao wa Tigo kutumia huduma ya Uber App bure kwenye
simu zao za mkononi bila tozo lolote la gharama za data. Uber ni mfumo
wa simu za kisasa unaowezesha watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi
nyingine kwa kubonyeza kitufe tu! Lengo kuu la Uber ni kuwezesha usafiri
salama, wa uhakika na kwa gharama nafuu kwa kila mtu, kila sehemu.
Makubaliano haya yatawahamasisha maelfu ya wakaazi wa Dar es Salaam
ambao wamejisajili na mtandao wa Tigo kutumia Uber App kwa ajili ya
huduma za usafiri jijini Dar es Salaam,’ Msemo alibainisha.
Kampuni
hizi mbili zitashirikiana katika bidhaa na promosheni zitakazoboresha
huduma kwa wateja wa sasa na wa siku zijazo. Tigo na Uber nchini
Tanzania wanatarajia kutangaza ofa zaidi kabambe zitakazowawezesha
wateja kufurahia huduma za Uber jijini Dar es Salaam ambapo huduma za
Uber zinapatikana kwa sasa.
……………………………………………………
No comments :
Post a Comment