Mafunzo
hayo ya siku tatu yamefanyika katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo
katika ofisi za manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na wanawake na
vijana 60 kutoka vikundi 20 vya wajasiriamali ambao wamepata mikopo ya
shilingi milioni 125.
Akizungumza
wakati wa kufunga mafunzo hayo leo Jumatatu Machi 19,2018 Matiro
aliwataka vijana na wanawake hao kutumia fedha walizopewa kwa malengo
waliyokusudia na kuhakikisha wanaanzisha viwanda vidogo vitakavyoinua
uchumi wao.
“Tumieni
mikopo hii kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo ili kumuunga mkono rais
wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli anayetaka Tanzania iwe nchi ya
viwanda,pale mnapokwama tafadhali wasilianeni na viongozi wa
serikali,tutawasaidia na pia tutatembelea miradi yenu ili tujue
mnachofanya”,alisema Matiro.
Aidha
aliwataka vijana na wanawake kujitokeza kwa wingi kuomba mikopo kwenye
halmashauri za wilaya ,mikopo ambayo haina masharti magumu wala riba
kubwa ukilinganisha na taasisi za kifedha (benki).
“Msikubali
kukata tama kwamba maisha ni magumu,hata siku moja serikali haiwezi
kugawa pesa kwa mtu mmoja mmoja,anzisheni vikundi vya ujasiriamali,kisha
ombeni mikopo kwenye halmashauri,pesa zipo”,aliongeza Matiro.
Kaimu
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone alisema
vikundi hivyo vimepata mkopo wa shilingi milioni 125 kutoka mfuko wa
wanawake na vijana ikiwa ni asilimia 10 ya mapato ya ndani ya manispaa
hiyo.
“Katika
mwaka wa fedha 2017/18 manispaa imelenga kutoa shilingi milioni 208 kwa
ajili ya vijana na wanawake,katika awamu hii ya kwanza tumetoa shilingi
milioni 125 kwa vikundi 11 vya wanawake na 9 vya vijana”,alieleza
Kiwone.
“Baada ya
kutoa mikopo hiyo,tumeona ni vyema tuwape elimu ya kuhusu namna ya
kunufaika na mikopo,mafunzo yamedumu kwa muda wa siku tatu,na kipaumbele
cha manispaa ya wajasiriamali kuanzisha viwanda vidogo
vidogo”,aliongeza Kiwone.
Kwa
upande wake, Afisa Maendeleo ya vijana Manispaa ya Shinyanga,Charles
Luchagula alisema manispaa hiyo inaendelea kupokea maombi ya mikopo kwa
vijana na wanawake ili kujiinua kiuchumi na kujikimu kimaisha.
Nao
washiriki wa mafunzo hayo walisema kupitia mafunzo hayo ya siku tatu
wamepata elimu kuhusu namna ya kuanzisha biashara na kutafuta
masoko,kutengeneza mnyororo wa thamani kutunza kumbukumbu na vifungashio
na umuhimu wa uwekaji lebo.
Walisema
pia wamejifunza taratibu za utoaji wa mikopo na urejeshaji wa
mikopo,wajibu wa kiongozi wa kikundi,ukweli kuhusu Ukimwi,ukatili dhidi
ya wanawake na watoto pamoja na elimu kuhusu mfuko wa bima ya afya (CHF
iliyoboreshwa.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Washiriki wa mafunzo
kwa vikundi vya wajasiriamali vya wanawake na vijana wa manispaa ya
Shinyanga wakiwa wamesimama baada ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro kuingia ukumbini kwa ajili ya kufunga mafunzo hayo.Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro akiwasisitiza wanawake na vijana kutumia kwa malengo
yaliyokusudiwa pesa za mikopo walizopata
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiimba wimbo kuhusu wanawake ….”Wanawake wote hongeraa….”
Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Rajabu Masanja akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii
Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akielezea lengo la mafunzo hayo ya
siku tatu. Alisema lengo ni kuwajengea uwezo wanufaika wa mkopo huo
kutumia vizuri fedha walizopata.
Afisa Maendeleo ya vijana Manispaa
ya Shinyanga,Charles Luchagula akiwasisitiza wanawake na vijana kutumia
fedha walizopata kuanzisha viwanda vidogo.
Washiriki katika mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo hayo wakijaza mkataba wa mkopo waliopata katika kikundi chao
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
No comments :
Post a Comment