Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Mkuu wa
Wilaya ya Mbeya Mhe. Paul Ntinika (kulia) wakati wa ziara yake leo
Mkoani Mbeya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto mwenye miwani)
akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Paul Ntinika (kulia mwenye
miwani ) alipotembelea eneo la Game lililotumika kama kambi ya wapigania
uhuru wa Msumbiji leo Mkoani Mbeya wakati wa ziara yake kutembelea
maeneo ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika
Nyumba zilizopo katika eneo la
Game zilizotumiwa na wapigania uhuru wa Msumbiji ambazo kwa sasa
zinatumiwa na Idara ya Maliasili na utalii.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akimsikiliza Mratibu
wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi
Mduma (kulia) alipotembelea Nyumba ya Binti Matola aliyekuwa
mwanaharakati na rafiki wa Mwalimu Nyerere ambaye aliweza kumhifadhi
Hayati Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru wakati wa ziara yake
kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo Mkoani
Mbeya.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimsikiliza Afisa
utamaduni Halmashauri ya Mbeya Bibi. Nimwindaeli Mjema (mwenye koti
jeusi) alipotembelea Nyumba ya Juma Mtoto ambayo ilitumika kufanyika
vikao vya siri vya Hayati Mwalilmu Nyerere na wajumbe wake wakati wa
ziara yake kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo
Mkoani Mbeya.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa amesimama katika jukwaa
ambalo Mwalimu Nyerere alisimama kuhutubia wananchi lililopo katika
Uwanja wa mikutano uliokuwa ukitumiwa na Hayati Mwalimu Nyerere
kuendeshea mikutano wakati wa ziara yake kutembelea maeneo ya urithi wa
ukombozi wa Bara la Afrika leo Mkoani Mbeya
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye miwani) akimsikiliza
Bibi Martha Mapunda (katikati) alipotembelea nyumba za kwa Mapunda
ambazo bibi huyo alizitoa kwa wapigania uhuru wa msumbiji kuishi wakati
wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika.
Aliyekuwa mwalimu wa vita wa
Samora Machel na mwanajeshi mstaafu Joseph Mpewa (mwenye shati la
mistari) akizungumza na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati wa ziara yake
kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo Mkoani
Mbeya
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wanafunzi wa
Shule ya Sekondari ya Samora Machel ambayo hapo awali majengo yake
yalitumika kama kambi ya wapigania uhuru wa Msumbiji na Afrika ya Kusini
wakati wa ziara yake kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa Bara la
Afrika leo Mkoani Mbeya
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
………………
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameahidi kufikisha taarifa ya
hatua ambayo Tanzania imefikia katika harakati za kutafiti na kuhifadhi
kumbukumbu za ukombozi wa Bara la Afrika kwa mawaziri wa utamaduni wa
nchi za kusini mwa Afrika ili nchi hizo wanachama ziweze kuendelea na
hatua nyingine ya kuchangia katika ujenzi wa kituo cha kuhifadhi
kumbukumbu hizo.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo
leo Mkoani Mbeya alipofanya ziara kukagua maeneo yaliyotumika wakati wa
harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na kusema kuwa serikali ipo
katika mpango ambao maeneo yaliyotumika katika harakati za ukombozi wa
Bara la Afrika yatakarabati na kurejesha muonekano wake wa awali ili
yasipotezi historia.
“Majengo yaliyotumika katika
harakati za urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika ni sehemu ya historia
na maeneo muhimu sana ambayo yanatakiwa kuboreshwa ili yaweze kuendelea
kuwepo katika muonekano ule ule wa awali kwa lengo la kutokupoteza
historia yake” amesema Mhe. Mwakyembe
Aidha Mhe. Mwakyembe amesema kuwa
serikali imechukua wajibu wake wa kubaini maeneo yaliyotumika wakati wa
harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na kuwaomba viongozi wote nchi
nzima kuendelea kubaini maeneo na vitu vilivyotumika katika harakati za
ukombozi wa Bara la Afrika vilivyopo katika maeneo yao ili wizara
iyaendeleze kwa maslahi ya taifa na Afrika kwa ujumla
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Mbeya Mhe. Paul Ntinika ameitaka programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara
la Afrika kuzingatia na kuchukua taarifa ya vitu mbalimbali kama vile
vyakula vilivyotumika, vifaa na nyimbo zilizotumika kuhamasisha ukombozi
wa Bara la Afrika ili jamii ya sasa ifahamu kumbukumbu za ukombozi wa
Bara la Afrika kwa undani zaidi.
Naye Mratibu wa Programu ya Urithi
wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi Mduma amesema kuwa hadi
sasa programu inakusanya vitu vyote vilivyotumika wakati wa harakati za
ukombozi wa Bara la Afrika ambapo nyimbo 42 zilizokuwa zikihamasisha
mambo ya ukombozi zimekusanywa, hotuba 78 zilizotumika wakati wa
harakati za ukombozi zimepatikana, maeneo 161 yaliyotumika wakati wa
harakati za ukombozi yameainishwa na watu 201 wamehojiwa ambao kwa namna
moja ama nyingine wamepitia harakati hizo.
Baadhi ya maeneo yaliyobainika
Mkoani Mbeya kutumiwa na wanaharakati na wapigania uhuru wa Bara la
Afrika ni pamoja na eneo la Game, Nyumba ya Binti Matola, Nyumba ya Juma
Mtoto, Uwanja wa Mikutano, Sekondari ya Samora Michel, Nyumba iliyopo
Iyela iliyotumiwa na Samora Michel pamoja na Nyumba za kwa Mapunda.
No comments :
Post a Comment