Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu ili kuhakikisha kuwa
wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. Aidha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na
wadau wengine wa usalama na kufanikiwa kupata mafanikio makubwa ikiwa ni
pamoja na kukamata watuhumiwa mbalimbali wanaojihusisha na vitendo vya
uhalifu @ wakorea.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WANAOJIHUSISHA NA UHALIFU @ WAKOREA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
limefanya Operesheni maalum pamoja na misako katika maeneo mbalimbali ya
Jiji la Mbeya. Operesheni hii ililenga kukamata wahalifu mbalimbali
likiwemo kundi la vijana wanaojiita Wakorea ambao wamekuwa wakifanya
vitendo vya uhalifu na kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.
Operesheni hii imefanyika katika
maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya ambayo ni Ivumwe, Mwakibete,
Mwambene, Mama John, Ilomba, Mafiati, Makunguru, Iyela na Isyesye.
Katika Operesheni hii maalum,
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita
[06] kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kiuhalifu.
Watuhumiwa hao wamefahamika kwa majina ya:-
- KELVIN RAPHAEL [22] Mwakibete Bomba mbili ambaye ndiye kiongozi wa kundi hili la uhalifu @ Wakorea.
- CLEMENCE CHRISTOPHER @ MWAKALINGA [23] Mkazi wa Mwakibete Viwandani.
- CHARLES MWASUMBI [21] Mkazi wa Mwakibete
- EDGA EDWARD [20] Makondeko Mwakibete
- IPYANS NDUNGURU [21] Mkazi wa Mwakibete
- ADEN MWALUKASA [35] Mkazi wa Mwakibete
Pia katika Operesheni hii
maalum ya kuwasaka vijana wanaojihusisha na uhalifu hapa Jijini Mbeya,
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia vijana watatu [03] kutokana
na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uvunjaji nyakati za usiku na
mchana. Watuhumiwa hao wamefahamika kwa majina ya:-
- GODFREY JOSEPH @ MHENGA [20] Mkazi wa Ilemi Mapelele
- GODFREY PAUL @ MWAKASAJE [39] Mkazi wa Ilemi Mapelele
- MTEMI YAHAYA @ MWASANGA [42] Mkazi wa Uyole
Watuhumiwa hao baada ya kukamatwa na kupekuliwa walikutwa na vifaa mbalimbali walivyokuwa wakivitumia kuvunjia ambavyo ni:-
- Bisibisi – 03
- Nyundo – 01
- Mkasi – 01
Aidha watuhumiwa hao walikutwa na mali mbalimbali za wizi:-
- Flat Screen aina ya Home base
- Flat Screen aina ya Samsung
- TV ya kawaida aina ya Home base
- Sub Woofer 01
- Deck 03 aina ya Singsung 02 na Fusion 01.
Aidha mwanzoni mwa mwezi
Januari, 2018, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanikiwa kuwakamata
watuhumiwa nane [08] kutokana na kujihusisha na vitendo vya uhalifu
katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya ambao walifikishwa Mahakamani
na kwa sasa wanatumikia vifungo vya nje.
Pia watuhumiwa kumi na mbili
[12] ambao walikamatwa hivi karibuni katika Operesheni/Misako
iliyofanyika huko katika maeneo ya Ilemi, Juhudi, Makunguru na Mwenge
hapa Jijini Mbeya ambao kesi zao zinaendelea katika Mahakama ya Mwanzo
Iyunga
Watuhumiwa wengine watafikishwa Mahakamani mara tu baada ya Upelelezi kukamilika.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa vijana na
jamii kwa ujumla kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwani ni
kinyume cha sheria na badala yake wajishughulishe na kazi halali kwa
ajili ya kujipati kipato. Aidha anatoa onyo kali wafanyabiashara ya
vilezi kufuata sheria na taratibu za biashara yao ikiwa ni pamoja na
kufungua na kufunga sehemu zao za biashara muda sahihi kwa mujibu wa
sheria.
No comments :
Post a Comment