Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya
wadau wa Sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya
kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya
Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimuangalia
mtoto Salome katikati akinywa dawa ya Kifua Kikuu wakati wa uzinduzi wa
dawa ya kutibu kifua Kikuu kwa watoto wadogo leo jijini Dar es salaam,
kutoka kulia ni Mratibu wa Kupambana na Magonjwa ya Kifua Kikuu na Ukoma
Dkt. Beatrice Mutayoba, anayefuata aliyevaa kitenge ni mzazi wa Salome
Bi. Upendo Jeremiah.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akionyesha dawa
kutibu Kifua Kikuu kwa watoto wadogo wakati wa uzinduzi wa dawa hiyo leo
jijini Dar es salaam kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe
24 Machi 2019.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
Mohammed Bakari Kambi baadhi ya wadau wa Sekta ya afya hawapo pichani
wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo
kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019
iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wa Sekta ya afya
wakifuatilia kwa makini Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya
kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya
Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019 .
……………………….
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
SERIKALI kupitia Wizara ya
Afya imetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kununua mashine za kupima
vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu katika zahanati na vituo vya afya
nchini.
Hayo yamezungumzwa na Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
wakati wa uzinduzi wa dawa za kutibu ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa watoto
kuanzia umri wa miaka 14 kushuka chini leo jijini Dar es salaam.
“Serikali imadhamiria
kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu hivyo tumetenga shilingi bilioni 5
kwa ajili ya kuongeza mashine nyingine za kufanya uchunguzi kwa haraka
vya ugonjwa wa Kifua Kikuu zinazoitwa Genexpert ” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
marufuku kwa watoa huduma kutoa matibabu ya Kifua Kikuu kwa gharama
yoyote kwani huduma hiyo ni bure.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy
amesema kuwa marufuku kwa waganga wa kienyeji kuwashikilia wagonjwa wa
Kifua kikuu na badala yake wawaruhusu waende hospitali kwa ajili ya
msaada wa haraka.
Aidha, Waziri Ummy amesema
kuwa takribani watu laki moja na 60 wana maambukizi ya ugonjwa wa kifua
kikuu kwa makadirio ya mwaka 2016.
Sambamba na uzinduzi wa dawa
hizo Waziri Ummy amegawa mashine nyingne za Genexpert kwa ajili ya
kufanyia uchunguzi wa makohozi ili kugundua kuna maambukizi au hapana
kwa hospitali za ,Kairuki, Agakhan, Regency , TMJ na Indumandal ambazo
kila mashine moja inagharimu shilingi milioni 34 .
Aidha Waziri Ummy ametoa rai
kwa wazazi na walezi wa watoto kwenda hospitali mara wanapoona dalili
moja wapo ya TB ikiwemo kuumwa mara kwa mara kwa muda wa wiki mbili,
kukosa furaha, mtoto kulia mara kwa mara, kupungua uzito , kuchelewa
kukua na kikohozi cha mara kwa mara.
No comments :
Post a Comment