Monday, March 19, 2018

Serikali Kusambaza Umeme Vijiji Vyote Vilivyo kwenye Mpango Wa REA Kishapu


1
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Taraba wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea mradi wa umeme kijiji cha Negezi.
2
Baadhi ya wajumbe Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Negezi wakati ilipotembelea miradi ya umeme vijijini wilayani Kishapu.
3
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. ..akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji cha Negezi.
4
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa na viongozi wengine walipowasili kijiji cha Negezi kukagua miradi ya umeme.
5
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea miradi ya umeme.
6
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Shinyanga, …akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme wilayani Kishapu kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
7
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (kushoto) akishirikia kucheza ngoma ya Kisukuma akiwa akiwa kijiji cha Bulimba mabako umeme uliwashwa rasmi baada ya kukamilika usambazaji.
………………
Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu amesema Serikali itaendelea na usambazaji wa nishati ya umeme katika vijiji vyote 50 katika Wilaya ya Kishapu kama ambavyo iliahidi.
Amesema hayo wilayani humo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipofanya ziara wilaya Kishapu kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Kamati hiyo ikiwa kwenye vijiji vya Negezi na Bulimba ikiambatana pia na uongozi wa Mkoa na Wilaya, Mhe. Mgalu alisema kuwa mpango wa usambazaji umeme ni wa awamu na kuwa wananchi wasiwe na hofu kila kijiji kitafikiwa na mradi.
Aliongeza kuwa vijiji 33 kati ya 50 vitapata umeme wa REA awamu hii ya tatu wakati 17 vitapata nishati hiyo kupitia njia kuu inayounganisha mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Tabora.
Kwa upande wake, Kamati hiyo ya Bunge ilisema wataendelea kuikumbusha Serikali iendelee kutimiza ahadi zake kwa wananchi za kukamilisha miradi ya umeme.
Iliwataka wananchi ambao wamepitiwa na miradi hii katika vijiji vyao kuichangamkia fursa na kuomba kuunganishiwa ili kupata huduma hiyo na kujiletea maendeleo.
Aidha iliwataka wananchi kuboresha aina za makazi yao kadiri ya uwezo wao na kuezeka nyumba zao kwa bati na kuachana na matembe na hatimaye kuwa na nyumba zilizo bora.
Katika ziara hiyo kijiji cha Bulimba kilichopo kwenye kata ya Ukenyenge kumezinduliwa rasmi huduma ya umeme mradi uliokamilshwa kupitia REA na hivyo kutarajiwa kuwanufaisha wananchi.

No comments :

Post a Comment