Baadhi ya Mafundi wa Kampuni ya L
& T wakiwa kazini wakiendelea na shughuli ya kuunga na kufukia
mabomba ardhini kwa ajili ya kupeleka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa
Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri akizungumza na Mkandarasi na wananchi baada ya kutembelea na
kukagua mradi wa maji kutoka ziwa Victoria jana ambapo mradi huo unaotoa
maji katika Kijiji cha Solwa mkoani Shinyanga kupeleka mkoani Tabora
ambapo wilaya za Nzega,Igunga,Uyui na Tabora mjini zitanufaika na mradi
huo wa maji kutoka ziwa Victoria unaotekelezwa kwa muda wa miezi
thelathini.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Mamlaka ya Maji safi na Taka Manispaa ya Tabora (TUWASA) Mkama Bwire
akitoa ufafanuzi juu ya ulipaji fidia wakati utekelezaji wa mradi wa
maji kutoka Ziwa Victoria jana mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Aggrey Mwanri kutembelea na kukagua mradi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupulaakisisitiza
jambo kwa waandishi wa habari baada ya kuungana na Mkuu wa Mkoa wa
Tabora (hayupo pichani) kutembelea na kukagua mradi wa maji kutoka Ziwa
Victoria jana ambapo mradi huo unaotoa maji katika Kijiji cha Solwa
mkoani Shinyanga kupeleka mkoani Tabora ambapo wilaya za
Nzega,Igunga,Uyui na Tabora mjini zitanufaika na mradi huo wa maji
kutoka ziwa Victoria unaotekelezwa kwa muda wa miezi thelathini.
Picha na Tiganya Vincent
RS Tabora
………………………..
NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imesema
itamchukulia hatua kali mtu yoyote atakayebainika kuhujumu utekelezaji
wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Mkoani humo wenye gharama
ya bilioni 600 kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma ya maji safi na salama
kwa wakazi
wa eneo hilo.
Kauli hiyo imetolewa jana wilayani
Nzega na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wakati
alipotembelea na kukagua mradi huo unaotoa maji katika Kijiji cha Solwa
mkoani Shinyanga kupeleka mkoani Tabora ambapo wilaya za
Nzega,Igunga,Uyui na Tabora mjini zitanufaika na mradi huo wa maji
kutoka ziwa Victoria unaotekelezwa kwa muda wa miezi thelathini.
Alisema kuwa Serikali haitamfumbia
macho mtu yeyote atakayebainika kuwa na nia ovu ya kutaka kuiba vifaa
mbalimbali ambavyo vinatumiwa na wakandarasi katika kujenga mradi huo
ambao ni muhimu sana kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbali ya Tabora.
Mwanri alisema kuwa hadi sasa kazi
inaendelea ambapo Mkandarasi ya kampuni ya L & T yupo kazini
akiendelea na shughuli ya kuunga na kufukia mabomba ardhini na kueleza
kuwa hujuma yoyote ambayo inaweza kujitokeza inaaweza kusababisha mradi
kuchelewa kumalizika kusababisha wakazi wa maeneo ambao yalikuwa yapate
huduma hiyo kuendelea kupata matatizo ya maji.
Alisema kuwa kama kuna matatizo
yoyote wanayopata kama vile wizi wa vifaa ni vema wakaeleza ili uongozi
wa Mkoa uweze kuchukua hatua mapema kwa ajili ya kuendelea kuwawekea
mazingira mazuri ya ujenzi wa mradi huo na kuongeza kuwa kama watapata
matatizo na kunyamaza na muda wa kukamilisha mradi utafika wakiwa bado
hawajakamilisha Serikali haitasikiliza.
Mwanri aliwataka Wakuu wote wa
Wilaya na Watendaji wote ambapo mradi huo unapita kuhakikisha
wanasimamia ili isije ikatokee hujuma yoyote na kama ilitokea wakamate
watu wote wanatuhumiwa.
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji
Mkama Bwire alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo upo ndani ya
utekelezaji na tayari hata malipo ya fidia kwa wananchi waliopitiwa
maeneo yao na mradi yamekwishafanyika.
Alisema wananchi 204 ambao maeneo
yanapitiwa na Mradi huo na kukabainika kuwa wanatarajiwa kulipwa milioni
890.5 zitatumika kama fidia kwa wananchi hao
Alisema kuwa jumla ya milioni 760 zimeshalipwa kwa wananchi zaidi ya 162 ambao maeneo yao yalikwishafanyiwa tathmini.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya
Nzega alisema wananchi wa wilaya yake wanaupokea Mradi huo kwa furaha
kwa kukamilika kwake kutasaidia kuwaondolea tatizo la upatikanaji wa
maji safi na salama ya uhakika.
Mradi huu wa Maji unatarajia
kuwanufaisha wakazi wa Mkoa wa Tabora wapatao milioni moja ambao
watakuwa na uhakika wa maji safi na salama.
No comments :
Post a Comment