Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, Dkt. Juma Malewa(meza kuu mbele) akisaini Mkataba wa
makubaliano baina ya Asasi ya TECHNOSERVE katika mradi wa mafunzo ya
ujasiriamali kwa Wafungwa waliopo magerezani. Kulia ni Meneja Mkazi wa
Asasi ya hiyo Bw. Monsiapile Kajimbwa akisaini mkataba huo. Hafla fupi
ya utilianaji saini Mkataba huo umefanyika leo Machi 19, 2018 Makao
Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) na Meneja Mkazi wa Asasi ya
TECHNOSERVE, Bw. Monsiapile Kajimbwa(kulia) wakionesha nyaraka za
Mkataba wa makubaliano mara baada ya utiliananji wa mkataba huo wa
mradi wa mafunzo ya ujasiriamali kwa Wafungwa waliopo magerezani.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, Dkt. Juma Malewa akipongezana na Meneja Mkazi wa Asasi ya
TECHNOSERVE, Bw. Monsiapile Kajimbwa mara baada ya kubadilishana Mkataba
wa makubaliano baina ya Asasi hiyo katika mradi wa mafunzo ya
ujasiriamali kwa Wafungwa waliopo magerezani.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la
Magereza wakishuhudia utiliananji saini wa mkataba huo. Kulia ni
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, George Mwambashi kutoka
Divisheni ya Sheria ya Magereza(kushoto) ni Mrakibu Mwandamizi wa
Magereza, Uswege Mwakahesya ambaye ni Mratibu wa Programu za
Ujasiriamali katika Jeshi la Magereza
Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
………………
Na Lucas Mboje, Jeshi la Magereza;
Jeshi la Magereza limetiliana
saini makubaliano na Asasi ya TECHNOSERVE katika
kuendesha mafunzo ya
ujasiriamali kwa wafungwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 30
waliopo magerezani katika Mikoa ya nyanda za juu Kusini ikiwemo Mbeya,
Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi na Rukwa.
Hafla ya kutiliana saini
makubaliano hayo imefanyika katika Ofisi za Makako Makuu ya Jeshi la
Magereza jijini Dar es Salaam na Asasi ya TECHNOSERVE iliwakilishwa na
Afisa wake Bw. Monsiapile Kajimbwa.
Akizungumza baada ya kutiliana
saini makubaliano hayo, Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa
amesema kuwa mafunzo hayo ya ujasiriamali yatawapa uwezo wafungwa wa
kubaini na kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uwezo wa kubuni
na kuandaa mipango ya biashara.
“Mafunzo haya yatawanufaisha sana
wafungwa waliopo magerezani katika mikoa hiyo kwani yatawajengea uwezo
wa kujitambua pamoja na kujipatia vipato halali badala ya kutenda
uhalifu katika jamii.” Alisema Jenerali Malewa.
Ameongeza kuwa mafunzo hayo
yatafanyika katika Chuo cha Ufundi cha Magereza Ruanda kilichopo Mkoa wa
Mbeya ambapo wafungwa watajifunza nadharia na vitendo katika dhana
nzima ya ujasiriamali ikiwemo stadi za utengenezaji sabuni, ushonaji,
useremala, ufumaji sambamba na uandaaji wa mipango ya kibiashara.
Meneja Mkazi wa Asasi ya
TECHNOSERVE, Bw. Monsiapile Kajimbwa amesema kuwa hatua ya kutiliana
saini makubalino hayo ni kuimarisha ushirikiano kati ya Asasi yake na
Jeshi la Magereza katika kutoa mafunzo kwa wafungwa ili waweze kupata
ujuzi kupitia program hiyo.
Dira ya Jeshi la Magereza ni kuwa
Jeshi la kurekebisha wahalifu lenye utaalam wa hali ya juu
linaloendeshwa katika kanuni na viwango vilivyowekwa Kitaifa na
Kimataifa.
No comments :
Post a Comment