NA K-VIS BLOG/KHALFAN
SAID
SERIKALI imesema haitabadili msimamo wake wa kuwapeleka mahakamani waajiri wote ambao
bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia
Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amewaambia waandishi wa habari leo Machi 6, 2018 jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri ametoa tamko hilo wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya
wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekeleza
takwa hilo la Kisheria ikiwa ni pamoja na wale ambao hawateketelezi
inavyopasa Sheria ya ajira na mahusiano kazini.
Akiwa kwenye kiwanda cha kugandisha barafu cha Bhogal kilichoko
Chamazi, Naibu Waziri pia aliagiza kukamatwa mara moja wafanyakazi watatu raia
wa kigeni ambao walikutwa hawana vibali vya kufanyia kazi.
“Dar es Salaam kuna jumla ya waajiri 14,484, na kati ya hao, 6,907,
tumebaini bado hawajajisajili na nimewaagiza maafisa wa WCF kuwafikisha
mahakamani mara moja kuanzia kesho mashtaka dhidi yao yaandaliwe,”
Aliagiza Naibu Waziri Mavudne ambaye alifuatana na Kamaishna wa Kazi Bi. Hilda
Kabisa, na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi,
(WCF), Bi. Rehema Kabongo.
"Lakini pia nitoe wito kwa waajiri nchini, kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha
uratibu ajira za wageni, kinaelekeza kuwa hataruhusiwa mgeni yoyote kufanya
kazi nchini bila ya kuwa na kibali, na hawa tumewauliza vibali vyao hawakuwa
navyo kwa hivyo nimeagiza wakamatwe na wapelekwe polisi na kisha wafikishe
mahakamani.” Alisema Mhe. Naibu Waziri Mavunde.
Ziara ya naibu waziri ni muendelezo wa operesheni inayoendelea
nchini kote kuwabaini waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa
Wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na kuwabaini wale ambao hawatekelezi Sheria ya
ajira na mahusiano kazini.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bi. Rehema
Kabongo, alisema Mfuko umeanza kutekeleza maagizo ya serikali kwa kuwafikisha
mahakamani wale wote ambao bado hawajajisajili na Mfuko na kwamba wanakabiliwa na
adhabu ya kulipa faini isiyopungua shulingi Milioni 50, (Milioni Hamsini) au
kifungo cha miaka mitano jela au vyote kwa pamoja.
“Nitoe
wito kwa waajiri, operesheni hii ndio imeanza na kama
bado kuna mwajiri ambaye bado hajatekeleza wajibu wake asisubiri
kufikishwa
mahakamani, ni vema akatekeelza wajibu wake kwa kujisajili na
kiuwasilisha taarifa sahihi za shughuli zake kwenye Mfuko.” Alisema. 

Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia
Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(katikati), akizungumza jambo
wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kubaini waajiri ambao bado
hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), jijini Dar es
Salaam Machi 6, 2018. Wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji
wa Mfuko huo, Bi. Rehema Kabongo.
Mhe. Mavunde, na Bi. Rehema wakipitia nyaraka
Raia wa kigeni waliojuwa wafanyakazi wa
kiwanda cha kugandisha barafu, wakiwa kwenye gari kupelekwa kituo cha
polisi kwa kosa la kufanya kazi nchini bila kibali.
Raia
wa kigeni waliojuwa wafanyakazi wa kiwanda cha kugandisha barafu,
wakiwa kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa kosa la kufanya kazi
nchini bila kibali.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Uhusiano Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Bi. Laura Kunenge, (kushoto),
akizungumza jambo na Kamishna wa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Bi.Hilda Kabisama.
Afisa Mwajiri kiwanda cha Carmel
Concrete cha Mbagala Kizuiani akijieleza kwa Naibu Waziri Mavunde baada
ya kubainika kiwanda hicho kinakiuka Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini.
kwa kutowalinda wafanyakazi kwa kuwapatia vifaa vya kujihami.Kiwanda
hicho kimetozwa faini ya zaidi ya shilingi Milioni 10 kwa kosa hilo na
mengineyo.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughhulikia Kazi, Ajira na
Vijana, Antony Mavunde, (mwenye suti), akizunhumza jambo wakati alifanya
ziara ya kushtukiza kwenye kiwanda cha Carmel Concrete cha Mbagala
Kizuiani jijini Dar es Salaam jana (Machi 6, 2018), ili kubaini waajiri
ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), na
ambao hawatekelezi Sheria ya ajira na mahusiano kazini. Jumla ya waajiri 6,907 jijini Dar es Salaam, hawajajisajili na Mfuko na watapelekwa mahakamani.
![]() |
| Mfanyakazi wa kiwanda cha Carmel akilalamika mbele ya Naibu Waziri Mavunde, kuhusu mazingira mabovu ya kufanyia kazi na mishahara midogo kinyume na maelekezo ya serikali |
Naibu Waziri akiumuuliza mfanyakazi
huyo wa kiwanda cha kugandisha barafu, ambacho pia kimebainika kufanya
shughuli za kuchomelea vyuma, baada ya kumkuta hana viatu vigumu
(gumboots)
Naibu Waziri akiongozana na Kmaishana wa
Kazi, Bi.Hilda Kabisa na maafisa wengine wakati wakiwasili kiwanda cha
kugandisha barafu cha Bhogal, huko Mbagala Chamazi nje kidogo ya jiji.


No comments :
Post a Comment