Baadhi ya wasafiri na wakazi
wa Nyahua wilayani Uyui wakiwa katika eneo ambalo barabara imekatika
kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kukatika kwa
mawasiliano baina ya Itigi na Tabora. Nyuma ni basi dogo la Prince
Ramigo linalofanya safari zake kutoka Tabora kwenda Dodoma kupitia
Itigi.
Baadhi ya wasafiri kutoka
katika Basi la Prince Ramigo na wakazi wa Nyahua wilayani Uyui
wakijaribu kuvuka jana katika eneo ambalo barabara imekatika kutoka na
mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kukatika kwa mawasiliano
baina ya Itigi na Tabora. Nyuma ni basi dogo la Prince Ramigo
linalofanya safari zake kutoka Tabora kwenda Dodoma kupitia Itigi.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Tabora Mhandisi
Damian Ndabalinze akizungumza na waandishi wa habari na wasafiri jana
mara baada ya kutembelea eneo la tukio ili kujionea uharibifu wa
barabara ulitokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha kukatika kwa
mawasiliano baina ya Itigi na Tabora
Kamanda wa Kikosi cha Usalama
Barabarani Mkoani Tabora SP Emilian Kamuhanda akizungumza na waandishi
wa habari na wasafiri jana mara baada ya kutembelea eneo la tukio ili
kujionea uharibifu wa barabara ulitokana na mvua kubwa iliyonyesha na
kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora na kisha
kutoa tahadhari kwa Madereva kutodiriki kupita katika eneo hilo
Basi la Prince Ramigo
linalosafirisha abiria kutoka Dodoma kwenda Tabora likiwa limekwamwa
katikati ya maji jana mara baada ya Dereva kujaribu kupita.
Picha na Tiganya Vincent
……………..
NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo katika eneo la Nyahua wilayani Uyui Mkoani Tabora imesababisha kukatika kwa barabara kuu
ya Tabora kupitia Itigi hadi Dodoma na kusababisha magari ya abiria na
mizigo kwishindwa kuendelea na safari zake kwa kutumia barabara hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika eneo la tukio Meneja wa Wakala wa Barabara )TANROADS) Mkoa wa Tabora Mhandisi
Damian Ndabalinze alisema mvua zilizonyesha katika maeneo hayo
zimesababisha kukatika kwa eneo hilo ambapo ndipo barabara ya lami
inaishia.
Aliwataka madereva wa magari ya
aina yoyote kudiriki kupita katika aina hilo kwa sababu wanaweza
kuhatarisha maisha yao na abiria na mizigo.
Ndabalinze alisema dereva yoyote
atakayekaidi na kuamua kupita katika eneo hilo kwa kulazimisha jambo
lolote litakalompata itakuwa ni yeye kajisababishia na asilelekeze
lawama kwa chombo chochote.
Alisema wakati taratibu nyingine
zikiendelea za kutaka kurejesha mawasiliano kwa kutumia barabara hiyo ni
vema magari yote ya kuja na kutoka Tabora yakapitia barabara ya Manyoni
, Singida , Nzega hadi Tabora.
“Natoa wito kwa magari ya kwenda
Kigoma na yale yanayoishia Tabora yapitie Nzega ili kuepusha usumbufu
kwa abiria na kwa madereva …kwani njia hii haipitiki tena” alisema
Meneja huyo.
Naye Afisa Mfawidhi wa SUMTRA Mkoa
wa Tabora Joseph Michael alisema kutokana na tatizo la kukatika kwa
barabara hiyo anatoa ruhusa kwa magari yote yaliyokuwa yakipitia
barabara ya Tabora kupitia Itigi hadi maeneo ya Dodoma na Dar es salaam
kuzungukia Nzega bila kibali kwa siku ya leo.
Alisema baada ya hapo wamiliki wanatakiwa kutafuta vibali ikiwa kama hali ya barabara hiyo itachelewa ili kuepuka usumbufu.
Naye Kamanda wa Kikosi cha Usalama
Barabarani Mkoani Tabora SP Emilian Kamuhanda alisema wamejipanga
kutoka matangazo katika Stendi kuu ya mabasi Tabora na kushirikiana na
Kikosi ya Usalama Barabara cha Mkoa wa Singida ili kuwaelekeza madereva
wote wapiti njia ya Nzega ili kuepuka usumbufu.
Kwa upande wa Mtendaji wa Kata ya
Kizenge Maganga Saulo alisema mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo
ilikuwa kubwa na kusababisha kukatika kwa eneo hilo , hatua iliyopelekea
magari kushindwa kupita.
Alisema ili kuhakikisha hakuna maafa yatakayotokea wanatumia Jeshi la Akiba kuwazuia madereva wanaotaka kujaribu kuvuka.
Eneo la barabara lilikatika liko umbali wa Kilometa 79 kutoka Tabora Mjini.
No comments :
Post a Comment