Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (watu wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa
akitoa maelezo kuhusu masuala ya watu wenye ulemavu kwa Kamati ya Kudumu
ya Katiba na Sheria ili kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/18 na Makadirio ya Mapato na
Matumizi kwa mwaka 2018/19 Kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na
Sheria Machi 28, 2018 Bungeni Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akifafanua jambo wakati kikao cha Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Machi 28, 2018 Bungeni Dodoma.
Baadhi ya
Wajumbe wa kikao wakifuatilia mada zinazowasilishwa wakati wa Taarifa
ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/18 na
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19 Kwa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Katiba na Sheria Machi 28, 2018 Bungeni Dodoma.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe.Najma Giga akiongoza kikao
cha kamati yake wakati wa Uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa
Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/18 na Makadirio ya Mapato
na Matumizi kwa mwaka 2018/19 kwa mafungu 27,62,65 na 15 ya Ofisi hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akitoa hoja wakati wa Kikao cha Kamati hiyo.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kailima Ramadhan akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wa kikao wakifuatilia mada zinazowasilishwa wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA)
Na.MWANDISHI WETU
Serikali
imedhamiria kuboresha mazingira ya watu wenye ulemavu ili kuwasaidia
kujikwamua katika nyanja zote na kuchangia katika maendeleo nchini.
Hayo
yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
masuala ya watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa wakati wa Uwasilishaji wa
Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka
2017/2018 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/2019 kwa
mafungu ya Taasisi zinazosimamiwa na Ofisi hiyo Mjini Dodoma.
Waziri
Ikupa alieleza kuwa tayari Serikali imeanza mikakati ya kuboresha
mazingira ya watu wenye Ulemavu kwa kuvifufua vyuo na vituo vyao ili
kuwapa nafasi nzuri ya kujifunza katika mazingira yanayowapa uhuru na
tija kulingana na aina za ulemavu walionao.
“Tayari tumeanza
kuboresha mazingira ya vyuo vya ufundi ikiwemo kile cha Yombo kilichopo
Mjini Dar es Salaam na Sabasaba ili kusaidia kuwapa fursa za kujifunza
katika mazingira rafiki hii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuna kuwa na
vifaa vya kutosha”.Aliongezea
Sambamba na hilo Serikali
inaendelea na hatua za kuboresha mazingira ya Watu wenye ulemavu kwa
kuwajengea uwezo, kuongeza wataalam wa kuwafundisha, kuwapa mafunzo
maalumu yenye kuleta tija pamoja na kuwashirikisha katika fursa za
maendeleo.
Aliongezea kuwa Ofisi yake itaendelea kushirikiana na
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na vyuo mbalimbali ili
kupata taarifa sahihi za mahitaji halisi ya watu wenye ulemavu
yatakayosaidia kuwa na kanzidata ya kudumu yenye taarifa hizo.
“Jitihada
zilizopo ni pamoja na kushirikisha Wizara ya Elimu ili kuweza kupata
taarifa muhimu za watu wenye ulemavu zitazosaidia kuwa na kanzi data ya
uhakika inayowatambulisha kwa idadi, aina ya ulemavu na ujuzi alionao
ili kuwapa nafasi wenye sifa za kushiriki katika programu za kukuza
ajira”.Alisisitiza Mhe.Ikupa
Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa
Kamati hiyo Mhe.Amina Mollel alishauri kuwe na mikakati madhubuti yenye
tija kwa watu wenye ulemavu ikiwemo kutoa semina kwa watumishi wa
serikali juu ya namna bora ya kuwahudumia watu wenye ulemavu kwa
kuzingatia mahitaji yao.
“Ifike mahali kuwe na mikakati madhubuti
ya kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum hususani kwa kuwajengea uwezo
watumishi kujua namna nzuri ya kuwahudumia watu wenye ulemavu pamoja na
kusaidia kuzikabili changamoto wanazokabiliana nazo”.Alisema Mhe.Mollel.
Pages
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment