Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Bill na Melinda Gates Bw. Rodger Voorhies kwenye
Makazi ya Makamu wa Rais, Kilimani mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
…………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 23 Machi, 2018
amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Bill & Melinda Gates Foundation Bw. Rodger Voorhies kwenye makazi ya
Makamu wa Rais, Kilimani mjini Dodoma.
Makamu wa Rais amesema amezungumza
mambo mengi na Bw. Rodger hasa kwenye masuala ya afya, uwezeshaji
wanawake kiuchumi, kuwatoa kwenye kilimo cha sasa na kuwaingiza
kwenye
kilimo biashara lakini pia kuongeza thamani ya mazao na mambo ya masoko.
Makamu wa Rais alisema
wamezungumza namna ya kuwarasimisha wanawake wa vijijini na wanawake
wakulima ikiwa pamoja na uwezekano wa wanawake vijijini kuweza kupata
mikopo.
Aidha Makamu wa Rais alizungumzia
suala zima la upatikanaji wa maji safi na salama haswa kwa wakazi wa
jiji la Dar es Salaam ambapo mara kwa mara kumekuwa na milipuko ya
magojwa ya kipindu pindu.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation Bw. Rodger
Voorhies alisema wamekuja kwa Makamu wa Rais kuzungumza juu ya shughuli
zinazofanywa na taasisi hiyo hapa nchini haswa katika masuala ya Kilimo
na Afya na Mkakati Mpya wa Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.
Aidha wameipongeza Serikali ya
Tanzania kwa hatua kubwa ambayo wamepiga katika kuwajumuisha wanawake
katika masuala yanayohusu Fedha.
Mwisho, Mkurugenzi huyo ameahidi ushirikiano mkubwa kwa Serikali ya Tanzania katika kutekelezaji wa miradi ya taasisi yao.
No comments :
Post a Comment