Mkurugenzi Mkuu wa
MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akizungumza na waandishi wa habari
Dar es Salaam jana walipotembelea Bohari ya Dawa kujionea shughuli
mbalimbali zinazofanywa na bohari hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa
Ugavi, Byekwaso Tabula, akitoa maelezo kwa wanahabari jinsi vifaa tiba
na dawa zinavyohifadhiwa katika bohari hiyo.
Muonekano wa maboksi ya dawa jinsi yalivyopangwa ndani ya bohari iliyopo Makao Makuu ya MSD Keko jijini Dar es Salaam.
Dawa na vifaa tiba zikipelekwa kuhifadhiwa ndani ya bohari.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akiwaonesha waandishi wa habari vifaa mfuko
wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack). Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Ugavi, Byekwaso Tabula na Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa
Wateja na Shughuli za Kanda, Salome Malamia.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Salome Malamia, akiwaonesha wabahabari vifaa vilivyopo kwenye mfuko huo.
Mkurugenzi Mkuu wa
MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akimkabidhi mfuko wenye vifaa
hivyo mwandishi wa habari, Hilda Mhagama kutoka gazeti la Daily News.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean
Rugambwa Bwanakunu, akimkabidhi mfuko wenye vifaa hivyo mwandishi wa
habari, Saum Juma kutoka Kituo cha Televisheni cha TV One.
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya Dawa (MSD) imezidi kuboresha
huduma zake za Ununuzi, Utunzaji na Usambazaji dawa, vifaa tiba na
vitendanishi vya maabara hata kukidhi viwango vya ubora wa Kimataifa na
kupata ithibati ya ISO 9001:2015.
Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi
wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean
Rugambwa Bwanakunu ameeleza kuwa kampuni ya Kimataifa ya ACM LIMITED
ilifanya ukaguzi Makao makuu ya MSD pamoja na Kanda zake nane mwezi
Agosti 2017 na MSD ilionekana kufuata miongozo ya juu ya kimataifa na
matakwa ya mamlaka za udhibiti ubora nchini.
Katika mkutano huo, Bwanakunu pia
alieleza kuwa hali ya upatikanaji wa dawa muhimu(135) MSD imeimarika
na kufikia asilimia 90,huku kwenye vituo vya kutolea huduma za afya
nchini hali ya upatikanaji wa dawa ni kati ya asilimia 85 na 98.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD pia aliwaonyesha
waandishi wa habari Mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama
(Delivery Pack) ambao umepunguzwa bei kutoka shilingi 40,000 mpaka
shilinhi 21,000.
Amesihi taasisi, asasi, jumuiya na
wananchi kununua mifuko hiyo ya vifaa vya kujifungulia na kutoa msaada
kwenye vituo vya afya na hospitali ili kuunga mkono juhudi za serikali
za kuboresha huduma za afya nchini .
Katika mkutano huo Bwanakunu
aliwazawadia waandishi wa habari wawili ambao ni wajawazito mfuko huo wa
vifaa vya kujifungulia kwa ajili ya kujiandaa kwenda kujifungua.
No comments :
Post a Comment