Thursday, February 15, 2018

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO AKIKAGUA MIRADI YA UJENZI MKOANI TANGA


1.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akikagua ujenzi wa nyumba ya makazi ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania iliyopo eneo la Pongwe katika Halmashauri ya Jiji la Tanga ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya sekta ya ujenzi inayotekelezwa na Wizara yake jana Jumatano Februari 14, 2018. Nyuma yake ni Meneja wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA) Mkoa wa Tanga, Edward Ngowi.
2.Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akipata maelezo kuhusu hatua mbalimbali za ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mkoa wa Tanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua  miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi  inayosimamiwa na Wizara katika Mkoa wa Tanga hapo jana Jumatano Februari 15, 2018.
3.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akipata maelezo kuhusu hatua mbalimbali za ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mkoa wa Tanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua  miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi  inayosimamiwa na Wizara katika Mkoa wa Tanga hapo jana Jumatano Februari 15, 2018.
4.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Luiza Mlelwa (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Wilaya kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa  (mbele) wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi inayosimamiwa na Wizara yake juzi Jumanne Februari 13, 2018.
5.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Luiza Mlelwa akimakabidhi taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya hiyo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na Wizara yake juzi Jumanne Februari 13, 2018.
6.Mbunge wa Muheza, Adadi Rajabu (aliyesimama) akizungumza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (mbele) aliyefika katika Wilaya hiyo kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi inayosimamiwa na Wizara yake juzi Jumanne Februari 13, 2018
7.
Mbunge wa Muheza, Adadi Rajabu akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa (shati nyeupe) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Muheza-Amani kwa kiwango cha lami wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi ikiwemo barabara inayosimamiwa na Wizara yake.
8.Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Kata ya Zirai iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi ikiwemo barabara juzi Jumanne Februari 13, 2018.
9.Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Zirai iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga wakifuatilia kwa makini mkutano wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Viongozi na wananchi wa Kata hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi ikiwemo barabara juzi Jumanne Februari 13, 2018.
11.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa mwenye (shati nyeupe) akisalimiana na Madiwani wa Kata ya Mombo iliyopo katika Halmashauri ya Korogwe  Vijijini wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Stephen Ngonyani (katikati) wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya ujenzi ikiwemo barabara jana Jumatano Februari 14, 2018.
12.Diwani wa Kata ya Mombo, Halima Mussa akizungumza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa (wa pili kulia) wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya sekta ya ujenzi ikiwemo barabara katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Mombo ikiwemo stendi ya Mombo jana Jumatano Februari 14, 2018. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyan
13.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (katikati) akiongozwa na Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani (wa pili kulia) na Diwani wa Kata ya Mombo, Halima Mussa (kushoto) kukagua kipande cha barabara kilichopo katika stendi ya Mombo ikiwa ni sehemu yake ya kukagua miradi ya barabara katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tanga jana Jumatano Februari 14, 2018.
14.Diwani wa Kata ya Mombo iliyopo Korogwe Mkoani Tanga, Halima Mussa akimpa maelezo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (kulia) kuhusu kuharibika kwa mtaro wa kupitisha maji machavu na uchakavu wa miundombinu ya barabara katika eneo la soko lililopo katika stendi ya Mombo Wilayani Korogwe jana Jumatano Februari 14, 2018. Wa pili kushoto ni Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani.

No comments :

Post a Comment