Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Enock Yakobo akieleza juu ya Ujenzi wa mradi wa barabara ya
Bariadi-Maswa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.
Makame Mbarawa wakati wa ziara yake katika eneo la ujenzi wa Kambi ya
Mkandarasi CHICCO anayetekeleza mradi huo Mkoani Simiyu.
Mjumbe wa Halmashuri Kuu ya CCM
(NEC), Gungu Silanga akimweleza jambo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa wakati wa ziara yake katika eneo la
ujenzi wa Kambi ya Mkandarasi CHICCO anayetekeleza mradi wa Ujenzi wa
Barabara ya Bariadi- Maswa Mkoani Simiyu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kulia) wakichota udongo na makoleo kujazia
sehemu inapojengwa Kambi ya Mkandarasi CHICCO anayetekeleza mradi wa
Ujenzi wa Barabara ya Bariadi Maswa wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
‘
Mkuu wa Wilaya ya Itilima,
Mhe.Benson Kilangi akieleza juu ya Ujenzi wa mradi wa barabara ya
Bariadi-Maswa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.
Makame Mbarawa wakati wa ziara yake katika eneo la ujenzi wa Kambi ya
Mkandarasi CHICCO anayetekeleza mradi huo Mkoani Simiyu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza Samweli Jisena
mwananchi kutoka Kata ya Luguru akitoa malalamiko yake , wakati
alipotembelea eneo la ujenzi wa Kambi ya Mkandarasi CHICCO
anayetekeleza mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Bariadi- Maswa Mkoani
Simiyu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa ( wa tatu kulia) akitoa maelekezo kwa
Mkandarasi CHICCO anayetekeleza mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Bariadi-
Maswa wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa
Simiyu, Mhandisi.Albert Kent akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa(wa pili kushoto),
alipotembelea eneo la ujenzi wa Kambi ya Mkandarasi CHICCO
anayetekeleza mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Bariadi- Maswa wakati wa
ziara yake Mkoani Simiyu.
…………………………………………………………………..
Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amemuagiza Mkandarasi wa Mradi wa
Ujenzi wa barabara ya Bariadi-Maswa yenye urefu wa Kilomita 49.7
kukamilisha mradi huo Juni 2019.
Waziri Mbarawa amesema hayo
wakati alipotembelea Kambi ya Mkandarasi CHICCO anayetekeleza Mradi huo
iliyopo kata ya Luguru wilayani Itilima wakati wa Ziara yake Mkoani
Simiyu .
Amesema barabara hiyo
iliyopangwa kujengwa kwa miezi 24 kuanzia Mwezi Oktoba 2017, itajengwa
kwa gharama ya shilingi bilioni 86.9 na tayari Serikali imeshamlipa
Mkandarasi shilingi Bilioni 8.9.
Amemuelekeza Mkandarasi CHICCO
kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo na kuahidi kuwa Serikali itamsimamia
na kuhakikisha mradi huo unakamilika mwezi Juni 2019, jambo ambalo
limekubaliwa na Mkandarasi huyo.
“Tutahakikisha tunamsimamia
Mkandarasi masaa yote usiku na mchana ili barabara hii imalizike kwa
wakati na tutamlipa fedha kila anapoleta ‘certicate’ kazi hii isisimame
tena, nawaagiza TANROADS na Mkandarasi Mshauri kusimamia barabara hii
ili thamani ya fedha ionekane” alisema Mbarawa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kutekeleza ahadi aliyoitoa mwezi Januari
2017 katika ziara yake Mkoani humo, ambapo amebainisha kuwa kukamilika
kwa barabara hiyo kutaufungua Mkoa huo kibiashara.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Enock Yakobo ameshukuru juhudi zinazofanywa na Serikali kwa
mkoa huo kwa kuwa ulipoanzaishwa mwaka 2012 barabara zilikuwa
zinapitika kwa shida, lakini sasa wananchi wanatumia muda mfupi kwenda
maeneo mbalimbali, hivyo amesema barabara hiyo itakapokamilika nayo
itachangia kurahisisha usafirishaji.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
wananchi wa Kijiji cha Banya wilayani Itilima mahali inapojengwa Kambi
ya Mkandarasi CHICCO wamelalamikia suala la mkandarasi kuchukua vibarua
wa kufanya kazi za mradi nje ya Mkoa pamoja na malipo yasiyoridhisha
kwa wale waliopata nafasi ya kufanya kazi katika mradi huo
“Mhe. Waziri hivi ni sahihi
kweli barabara ijengwe hapa kwetu halafu vibarua watoke Mikoa mingine,
mimi naona siyo sawa tunaomba Serikali itusaidie na sisi wananchi wa
hapa tupate kazi; pia hata hawa wanaofanya kazi hapa malipo ni kidogo
elfu tano kwa siku haitoshi” alisema Samweli Jisena.
Waziri Mbarawa amemuagiza Meneja
wa TANROADS Mkoa wa Simiyu, Mhandisi.Albert Kent kuhakikisha kuwa
anasimamia suala la wananchi wa eneo la mradi kupewa kazi na mkandarasi
na upande malipo amewataka wafanyakazi kukubaliana na mkandarasi juu ya
malipo yao.
Ujenzi wa Barabara ya
Bariadi-Maswa ni ahadi ya Rais wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli
aliyoitoa Januari 11, 2017 akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani
Simiyu mara baada ya kufungua barabara ya Lamadi-Bariadi yenye urefu wa
Kilomita 71.8 mjini Bariadi.
No comments :
Post a Comment