Wednesday, February 14, 2018

WAZIRI KALEMANI AMWASHIA MOTO MKANDARASI ANAYESAMBAZA UMEME VIJIJI Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akitoa maagizo ya utekelezaji wa usambazaji wa umeme kwenye maeneo ya vijiji na Kata za Iparamasa pamoja Kalembela wakati alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mojo kati ya ziara zake za kukagua utekelezaji wa usambazaji wa umeme wa REA awamu ya tatu.


Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akisalimiana na baadhi ya viongozi pamoja na wananchi wakati alipowasili  kwenye viwanja vya kijiji na kata ya Iparamasa kwaajili ya kuzungumza na wananchi.


Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akiwatunza wanakwaya wa kwaya ya kijiji cha iparamasa.

Meza kuu ikiongozwa na viongozi mbali mbali akiwemo Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani.

Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji akielezea namna ambavyo wananchi wameendelea kupata changamoto kutokana na kukosa umeme kwa muda mrefu. 

Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa waziri wa Nishati ,Dk Medard Kalemani.

Na,Joel Maduka ,Chato


 
Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani amemwagiza mkandarasi
shirika la White City  Internationala mbaye anasambaza umeme wa rea
awamu ya tatu kwenye Vijini na kata za Iparamasa na Kalembela kuhakikisha
anafanya kazi hiyo kwa haraka zaidi ili kuwasaidia wananchi ambao wamekuwa na
kilio cha muda mrefu cha uhitaji wa nishati ya umeme.
Hayo aliyasema wakati alipokuwa kwenye ziara ya Kukagua na
kuangalia utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini  Wilayani Chato.
Ambapo Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji ,amemweleza Waziri wa
nishati ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo matatizo ambayo yameendelea
kujitokeza kutokana na kukosekana  kwa umeme kwenye  kata yake  na kwamba kwa sasa kuna nguzo ambazo zimekaa
kwa muda wa miezi mitatu bila ya kusambazwa kwa wananchi ambao wanashida na
huduma hiyo.
 Mmoja kati ya wananchi wa kata hiyo ,Bw Peter Mabula ameelezea
kukosekana kwa umeme ni chanzo kikubwa ambacho kinakwamish

No comments :

Post a Comment