Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi katika ufunguzi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, mapema leo jijini Dar es salaam, katikati ni Naibu waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimjulia hali moja ya mama aliyekuwa
akiuguliwa na mtoto wake, akifanya hivyo baada ya kuzindua jengo la mama
na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, kulia kwake ni Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakisalimiana na Mbunge wa Ilala Mhe.
Azan Zungu wakati wa Uzinduzi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika
Hospitali ya Amana, wa pili ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul
Makonda na wa mwisho ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa mama aliyekuwa akiuguliwa na mtoto
wake, akifanya hivyo baada ya kuzindua jengo la mama na mtoto lililopo
katika Hospitali ya Amana, kulia kwake ni Naibu waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
Picha ya pamoja ikiongozwa na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,
kulia kwake ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda.
……………..
SERIKALI yaendelea kuongeza vituo
vya Afya nchini ikiwa ni moja ya jitihada za Serikali za kuboresha
Huduma za afya nchini jambo litakalo saidia kupunguza msongamano wa
wagonjwa katika Hospitali za Wilaya na Mkoa kwa kuwa huduma zote
zitakuwa zimeishia kwenye ngazi ya Kata.
Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa
ufunguzi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana,
mapema leo jijini Dar es salaam.
“Kumekuwa na ongezeko kubwa la
vituo vya Afya nchini kutoka vituo vya Afya 6321 kwa mwaka 2010 hadi
vituo vya Afya 7680 kwa mwaka 2016, na kazi ya nyongeza inaendelea,
kwaiyo tunaamini vituo hivi vitaweza kupunguza msongamano katika
hospitali za Wilaya, pamoja na Hospitali za Mkoa”, alisema Mhe. Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa.
Mhe. Waziri Mkuu alisema kwamba
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
ametenga kiasi cha Zaidi ya Bilioni 100 ikiwa ni fedha za kuboresha
Vituo vya Afya nchini ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi katika
maeneo yote nchini.
“Tumeanza kuboresha Vituo vya Afya
kwa kujenga Wodi yakinamama wanaojifungua, thieta, wodi za magonjwa
yakawaida, maabara, tunaongeza na nyumba za watumishi, ili kila kituo
cha Afya kiwe na miundombinu hiyo ili utoaji huduma uwe rahisi” alisema
Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mhe. Waziri Mkuu aliendele kusema
kwamba Serikali imetumia Zaidi ya Bilioni 161 katika kuendelea kuboresha
Huduma za Mama na Mtoto kwa lengo la kuokoa Maisha ya mama na mtoto
jambo ambalo ni moja kati ya changamoto kubwa nchini.
Aidha Mhe. Waziri Mkuu alisema
kwamba Serikali imeendelea kuboresha Huduma za Afya kwa kutenga kiasi
cha shilingi Bilioni 129 kwaajili ya vifaa vya kuwezesha kundesha
shughuli za upasuaji katika kila kituo cha Afya ambacho kinaboreshwa.
Wakati akitoa taarifa ya Afya ya
Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda alisema kwamba wakina mama
126,164 walipata nafasi ya kujifungua katika vituo vya Afya, huku
wakinamama 202 ambao ni sawa na Asilimia 0.5 walilazimika kujifungua kwa
wakunga, na Asilimia 1.5 zaidi ya akinamama 1976 walijifungua njiani
wakielekea kupata huduma, idadi inayoonekana kuwa kubwa sana katika Mkoa
wa Dar Es salaam.
Idadi ya 2016 inaonesha Zaidi ya
akina mama 85 walikuwa wanapoteza Maisha kati ya kina mama 100,000
waliokuwa wanajifungua lakini kwa sasa tangu maboresho yafanyike ni
akina mama 57 kati ya akina mama 100,000 wanaojifungua ndio hupoteza
Maisha, huku mikakati thabiti yakupunguza vifo hivyo ikiendelea kuwekwa.
Mhe. Makonda aliendelea kusema
kwamba zaidi ya watoto ambao wanafanikiwa kuwa hai na kuwa salamakatika
kujifungua ni Zaidi ya watoto 126,712, na watoto 131 huzaliwa wakiwa
tayari wameshakufa, idadi hii ikilinganishwa .
Pia Mhe. Makonda alimshukuru
AMSONS GROUP ambayo imetoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Jengo hilo la
Mama na Mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana huku akiwataka Wadau
wengine kuiga mfano huo katika dhana ya kusukuma gurudumu la maendeleo
katika jamii zetu.
Nae Naibu waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani imeongeza
Bajeti ya Dawa kutoka Bilioni 30 mpaka sasa ni Bilioni 270 likiwa ni
ongezeko la Zaidi ya mara 9, huku Wastani wa upatikanaji wa dawa ukiwa
Zaidi ya asilimia 80.
“Serikali wakati inaingia
madarakani Bajeti ya dawa ilikuwa ni Bilioni 30, mwaka unaofuata
ikafikia Bilioni 200, na hivi tunavyoongea Bajeti ya Dawa ni Bilioni
270, likiwa ni ongezeko la mara 9, kama msaidizi wako nasimama kifua mb
No comments :
Post a Comment