Wednesday, February 21, 2018

WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA DAWA ZA KULEVYA


PMO_9568
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa jiji la Mwanza baada ya kuwasili kwenye hospitali ya Sekou Toure kuzindua kliniki ya Methadone kwa ajili ya waathirika wa dawa za kulevya, Februari 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_9621
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Kamishina Jenerali wa mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Siyanga wakati alipozindua kliniki ya Methadone kwa ajili ya waathirika wa dawa za kulevya kwenye hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza Februari 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_9632
Baadhi ya waathirika wa dawa za kulevya wanaohudumia na Kliniki ya Methadone  iliyopo katika hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua kliniki hiyo, Februari 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_9651 PMO_9671 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Muongozo wa Uendeshaji wa Nyumba za Waathirika wa Dawa za Kulevya (Sober House) kwenye hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza, Februari 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wakiwemo wakazi wa mkoa wa Mwanza kuachana na biashara ya dawa za kulevya.
Pia Waziri Mkuu amegiza vijana nchini waelimishwe madhara mbalimbali yanayosababishwa na matumizi ya dawa za kulevya ili wajiepushe nazo.
Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumanne, Februari 20, 2018) alipozindua kliniki ya methadone kwa ajili ya waathirika wa dawa za kulevya.
Alizindua kliniki hiyo iliyopo kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure akiwa katika siku ya sita  ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.

“Serikali imejizatiti katika vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya, hivyo nawataka wananchi wasijishughulishe nayo. waache kutumia, kusambaza na kuuza.”
Pia aliwaomba wananchi washirikiane na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na dawa hizo.
Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers Siyanga  aliishukuru Serikali kwa kutambua madhara ya dawa za kulevya na kuchukua hatua.
Bw. Siyanga alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa waathirika wa dawa za kulevya kwenda katika kliniki za methadone ili wapatiwe matibabu yatakayowafanya kuachana na matumizi ya dawa hizo.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella alisema kuwa, mkoa huo ni miongoni mwa waathirika wakubwa wa biashara ya dawa za kulevya. Aidha, aliongeza kuwa bado kuna watu wanaoendeea kujishughulisha na biashara hiyo na kwamba Mkoa unaendelea kupambana nao.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile alisema dawa za kulevya zinasababisha madhara makubwa katika sekta ya afya kwa kuwa yanachangia kusambaa kwa magonjwa mbalimbali yakiwemo ukimwi na kifua kikuu.
Pia alisema kwa sasa dawa za methadone zinazotolewa kwa waathirika wa dawa za kulevya wanazipata kutoka kwa wahisani mbalimbali. Hata hivyo, Serikali imepanga kuingiza suala hilo katika bajeti ijayo ili ianze kuagiza y

No comments :

Post a Comment