Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa
Mwandoya jimbo la Kisesa wilaya ya Meatu mkoani Simiyu. (Picha na Ofisi
ya Makamu wa Rais)
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassa amewataka Viongozi wa mkoa
na wilaya mkoani Simiyu kusimamia sheria na kutowafumbia macho wanaowapa
mimba wanafunzi.
Akizungumza na Wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwandoya Kisesa, wilayani Meatu.
Makamu wa Rais alisema “Jamani
mnadhulumu watoto wetu hapa kuna kina Samia wa baadae mnapokuja kuwapa
ujauzito mapema mkawavunjia safari zao, mkawaoa mapema, wakina Samia
hawataibuka Meatu, tutatoka huko nje tutaibuka hapa Meatu, tunataka
Samia atoke hapa Meatu waachieni wasome, masuala ya mimba za utotoni
wapunguzieni.”
Makamu wa Rais aliwahimiza wananchi kujiandikisha kwa wingi kwenye mifuko ya bima ya afya kwani inafaida kubwa sana.
“Magonjwa yaweza kukufika wakati
huna pesa na kitu pekee kitakachokusaidia ni bima yako ya afya hivyo
wananchi hakikisheni mnapovuna na kuuza mazao yenu mnapata bima ya afya”
Makamu wa Rais aliwapongeza
wananchi wa Wilaya ya Meatu kwa kulima pamba kwa wingi ambapo wilaya
hiyo inategemea kilo 84 na kuwaahidi wananchi hao kuwa dawa za kuulia
wadudu zitapatikana kwa wingi kuanzia mwisho wa mwezi huu kwani serikali
imetoa fedha zaidi ya bilioni 9 .
Makamu wa Rais aliwaambia
wananchi hao kuwa barabara zote ambazo ilani ya uchaguzi imeahidi
kuzijenga zitajengwa na zile ambazo hazipo kwenye ilani ila zina umuhimu
zitaingizwa kwenye bajeti ijayo.
Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la
Kisesa Mhe. Luaga Mpina alisema kuwa kati ya kata 13 ni vijiji vine tu
vina maji hivyo alimuomba Waziri wa Maji kusaidia zaidi upatikanaji wa
maji.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe aliahidi kusimamia kwa ukamilifu upatikanaji wa maji .
No comments :
Post a Comment