Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru
Taratibu akieleza jambo wakati wa Mkutano wa wataalamu wanaounda
Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, uliojikita katika ulinzi na
usalama wa vimelea hatarishi leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini
Morogoro.
Mtaalamu
Masuala ya Mpango Mkakati wa Maabara kutoka Shirika la Maabara
–SANDIA, Laura Jones, akifafanua umuhimu wa Mpango huo wakati wa
Mkutano wa wataalamu wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini,
uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi leo tarehe 28
Februari, 2018 mjini Morogoro.
Baadhi
ya Wataalamu wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini,
wakijadiliana namna ya kuandaa Mpango Mkakati wa ulinzi na usalama wa
vimelea hatarishi, leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.
Wataalamu
wa Afya moja wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano wa kuandaa Mpango
Mkakati wa ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, leo tarehe 28
Februari, 2018 mjini Morogoro.
…………………….
Na. Mwandishi Maalum.
Wataalam wa Afya moja nchini ambao
ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo
pamoja na mazingira wameanza kuandaa Mpango Mkakati wa ulinzi na
usalama wa vimelea hatarishi utakaosaidia kuimarisha ulinzi na usalama
wa sampuli za vimelea hivyo hatarishi kutoweza kueeneza magonjwa kwa
binadamu.
Mpango huo utatoa mwongozo wa
namna sekta za Afya nchini ambazo ni sekta ya Afya ya
binadamu, Afya ya
wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira kushirikiana katika
kuvichukua vimelea kwa wanyama, binadamu na mimea au wakati wa
kuvisafirisha na kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi na wakati wa
kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.
Akiongea wakati wa Mkutano wa
wataalamu wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, leo tarehe 28
Februari,2018 mjini Morogoro, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa
Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu alibainisha kuwa serikali
imedhamiria kuijenga jamii yenye Afya bora kwa kuikinga na majanga
yatokanayo na magonjwa ya mlipuko hivyo imeamua kuandaa mpango huo ili
kuboresha uratibu.
Naye mratibu wa Mkutano huo
anayeshughulikia masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi
katika wizara ya Afya, Jacob Lusekelo, alibainisha mpango huo ambao
utatoa mwongozo wa sekta za Afya kushirikiana utasaidia kupunguza
maabukizi ya vimelea hivyo kwa wanyama na binadamu.
Tarehe 13 Februari 2018, Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua
Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na
lengo la kusimamia na kuratibu shughui za Afya moja nchini, ikiwemo
wataalamu wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, ambao
unawajumuisha wataalamu wa kutoka katika sekta zote za afya katika
masuala ya maabara.
Afya Moja ni dhana inayojumuisha
sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na mazingira katika
kujiandaa , kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu
,wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo Idara ya Uratibu Maafa
Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja kwa
kushirikiana na Shirika la Maabra SANDIA na DTRA wameandaa mkutano
wataalam hao.
No comments :
Post a Comment