WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amemuagiza kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mtwara Bw. Stephen Mafipa
kumtafuta popote alipo na kumkamata aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Mji wa Masasi Bw. Fortunatus Kagoro kwa tuhuma za matumizi mabaya
ya fedha.
Mbali na Bw. Kagoro pia Kaimu
Mweka Hazina Bw. Heri Hamad Afisa Mipango Bi Teresia Nsumba nao
ameagiza wakamatwe na baada ya uchunguzi watakaobainika kwamba
hawajahusika na ubadhilifu huo watarudishwa kazini. “Lazima fedha za
Serikali zitumike kama ilivyokusudiwa.”
Watendaji hao wanadaiwa kutumia
sh. bilioni 1.8 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa jengo la
Halmashauri ya Mji wa Masasi kwa kuchora mchoro na kujenga msingi
katika maeneo mawili tofauti.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo
(Jumatatu, Februari 26, 2018) wakati akizungumza na watumishi na
Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Masasi na Halmashauri ya wilaya ya
Masasi akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara.
Amesema mwaka 2014 Serikali
ilipeleka sh milioni 575 wilaya Masasi kwa ajili ya ujenzi wa jengo la
Halmashauri hiyo na fedha hizo ziliishia kutumika katika hatua za
maandalizi ya awali ikiwa ni pamoja na kutengeneza michoro ya jengo.
Waziri Mkuu amesema 2016/2017
Serikali ilipeleka tena sh. bilioni 1.25 kwa ajili ya ujenzi huo, ambapo
Halmashauri hiyo ilienda kutafuta eneo lingine na kufanya tena shughuli
zilizokuwa zimefanyika na kuanza ujenzi ambao umeishia katika msingi na
fedha zimeisha.
Pia amewataka watendaji hao
kutotumia fedha za makusanyo ya ndani kwa ajili ya kuziba pengo la fedha
za mradi huo ambazo baadhi yake hazijulikani zilipo na amewaagiza
Madiwani kutoruhusu jambo hilo.
“Madiwani msikubali kutumia fedha
za makusanyo ya ndani kupeleka kwenye ujenzi wa miradi ya maendeleo
ambayo tayari Serikali ilishatoa fedha ya ujenzi wake.
Amesema Serikali inahitaji kuona
fedha za maendeleo zinazopelekwa katika Halmashauri mbalimbali nchini
zinatumika kama ilivyoelekeza na si vinginevyo na Serikai haitakuwa na
mzaha kwa mtumishi atakayezitumia vibaya.
No comments :
Post a Comment