Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi, watendaji katika Sekta ya
Afya pamoja na wadau mbalimbali wa Afya mkoani humo katika kikao maalum
kilichofanyika kwa lengo la kutathmini mchango wa wadau wa
Afya(mashirika mbalimbali yanayofanya kazi na mkoa huo) ambacho
kilichofanyika Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,
Ndg.Jumanne Sagini akifafanua jambo katika kikao kati ya Viongozi wa
Mkoa huo , watendaji wa Sekta ya Afya ngazi ya mkoa na Wilaya na wadau
mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mratibu wa Mpango wa Kudhibiti
UKIMWI Mkoa wa Simiyu, Dkt.Khamisi Kulemba akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa mpango huo Mkoani humo katika kikao kati ya Viongozi wa
Mkoa huo , watendaji wa Sekta ya Afya ngazi ya mkoa na Wilaya na wadau
mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa
Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya
Mkoani humo wakifuatilia mada mbalimbali katika kikao cha tathmini ya
mchango wa wadau mbalimbali wa Afya Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini
Bariadi.
Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA), Bi.
Christine Mwanukuzi Kwayu akichangia jambo katika kikao kati ya
Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau
mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirikala Cuso
International Tanzania, Ndg.Romanus Mtung’e akichangia jambo katika
kikao kati ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na
wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa
Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya
Mkoani humo wakifuatilia mada mbalimbali katika kikao cha tathmini ya
mchango wa wadau mbalimbali wa Afya Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini
Bariadi.
Shekhe wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud
Kalokola akichangia jambo katika kikao kati ya Viongozi wa Mkoa wa
Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya
kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo
Mkoa wa Simiyu (CCT), Mchungaji Martine Samson Nketo akichangia jambo
katika kikao kati ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya
Afya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na
wadau (mashirika) mbalimbali wa Sekta ya Afya wanaofanya kazi na Mkoa
huo mara baada ya kufungua kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.
………………
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka amewataka wadau na mashirika mbalimbali wanaofanya kazi na
Mkoa huo katika sekta ya Afya kuelekeza fedha zao zaidi katika masuala
yanayojibu mahitaji ya wananchi wa Mkoa huo kwenye Afya badala ya
kujikita zaidi katika kugharamia mafunzo na semina kwa watumishi.
Mtaka ameyasema hayo katika
kikao kilichofanyika Februari 26, Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya
tathmini ya mchango wa fedha za wahisani na wadau mbalimbali wa sekta ya
Afya mkoani Simiyu na matokeo yake katika mahitaji halisi ya Kiafya
kwa wananchi.
Mtaka amesema mkoa huo una
wadau wengi wanaounga mkono juhudi za Serikali katika sekta Afya na
wanatoa fedha nyingi ambazo zikiwekwa pamoja na fedha zinazotengwa na
Serikali kupitia bajeti za Halmashauri zinaweza kujibu mahitaji ya mkoa
huo ambayo ni pamoja na upungufu wa zahanati na vituo vya Afya
“ Msingi mkubwa wa kikao hiki ni
kutaka tufanye tathmini ya fedha zinazotolewa na wadau ndani ya mkoa
wetu, kwa mwaka huu kwenye Halmashauri zetu tumetenga Bilioni 33.4 na
tuna shilingi bilioni 11 kutoka kwa wadau kwa ajili ya sekta ya afya,
hivi ‘impact’(matokeo) ya hizi bilioni 11 iko wapi? Natamani hapa kila
mwenye fedha yake atuambie mwaka huu atafanya nini” alisema Mtaka.
“Nashukuru TAMISEMI mko hapa hili
ni la kuliangalia , kama tunaingia mikataba ya shilingi bilioni 11 kwa
mwaka na mashirika yanayofanya kazi za Afya ndani ya Mkoa kwa ajili ya
kuwajengea uwezo watumishi, uhamasishaji na semina, wakati tukiwa
kwenye mazingira ambayo hatuna hata nusu ya idadi ya zahanati na vituo
vya afya vinavyohitajika ni lazima tutafakari wote” alisisitiza Mtaka.
Wakati huo huo Mtaka ametoa wito
kwa wataalam wa Afya kuendelea kutoa elimu na kuwahamasisha wananchi
kuzingatia uzazi wa mpango na akasisitiza umuhimu wa kutoa elimu kwa
wazazi watarajiwa (vijana) ili waanze kufanya maandalizi mapema juu ya
maamuzi ya idadi ya watoto watakaoweza kuwahudumia baadaye.
Naye Katibu Tawala Mkoa Simiyu,
Ndg.Jumanne Sagini amesema malengo waliyojiwekea katika kikao hicho ni
pamoja na kuhakikisha kazi zinazofanywa na wadau wa Afya mkoani humo
zinajibu matatizo ya Wanasimiyu na namna ya kuwa na uratibu mzuri wa
shughuli zao, mambo ambayo yamepokelewa na wadau hao na kuahidi kuweka
uratibu mzuri ili kuimariasha afya za wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi
wa Shirikala Cuso International Tanzania, Ndg.Romanus Mtung’e amesema
wadau wa Afya Mkoani humo watashirikiana na Viongozi na Wataalam wa Afya
katika kuweka mipango ya baadaye na watazingatia vipaumbele ambavyo
vitaleta matokeo chanya yanayoonekana kwa wananchi mkoani humo.
Kikao cha wadau wa Afya na
Viongozi Mkoa Simiyu kimewahusisha Viongozi na Wataalam wa Afya ngazi ya
Mkoa na Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala wa Wilaya,
Viongozi wa Dini pamoja na wadau(mashirika) wa Afya wanaofanya kazi na
mkoa wa Simiyu wakiwemo AMREF, AGPAHI, CUAMM, UNFPA, Mkapa Foundation,
AMERICARE, PSI,Red Cross, ICAP, TAMA, INTRAHELTH, WORD VISION, BORESHA
AFYA, CHAI, MARIESTOPES na BRIDGE2 AID.
No comments :
Post a Comment