MAHAKAMA
ya Wilaya ya Dodoma imemuamuru Mkuu wa Gereza la Isanga kumpeleka
hospitali kuu ya magonjwa ya akili (Mirembe), mkazi wa Kijiji cha
Nong’ona, Onesmo Machibya maarufu kama (Nabii Tito), ili kuchunguzwa
kama ana ugonjwa wa akili au la.
Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo,
James Karayemaha, amesema anahitaji majibu hayo Machi 5, mwaka huu siku
ambayo mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani ikiwa ni baada ya agizo la
kupimwa akili kutotekelezwa hapo awali.
Nabii Tito Machibya alifikishwa
mahakamani hapo akituhumiwa kufanya uchochezi wa kidini kupitia
mafundisho anayoyatoa na amekuwa akiieleza mahakama kuwa amekuwa
akifanya hivyo kwa sababu ana matatizo ya akili na kutoa vithibitisho
kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili.
No comments :
Post a Comment