Na Kijakazi Abdalla Maelezo
Hali ya Upatikanaji wa mafuta
utaendelea kuwa wa kawaida baada ya meli ya United Sprit 1 iliyokuwa
imechukuwa mafuta kuanza kushusha na kusambazwa vituoni tekea jana .
Akizungumza na Waandishi wa habari
huko katika Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati
Zanzibar (ZURA) Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa wateja Mussa Ramadhani Haji .
Amesema kuwa hali iliyojitokeza ya
upungufu wa mafuta kwa takribani wiki mbili zilizopita hasa katika
vituo vinavyomilikiwa na United Petroleum (UP) inatokana na meli ya
kampuni ya
United Petroleum kuwa ilikuwa katika foleni ya kusubiri
kupakia mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.
Aidha amesema kuwa Meli ya MT
Ukombozi ya Kampuni ya GAPCO nayo imefanikiwa kupakia mafuta ya Petroli
na Dizeli jana jioni katika Bandari ya Dar es Salaam na imefika Zanzibar
jana na mafuta na kushushwa na kusambazwa vituoni leo.
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi huyo
alisema kuwa Zura itaendelea kusimamia zoezi la usambazaji na uuzwaji
wa mafuta vituoni kwa kufuata taratibu za mamlaka.
Vilevile aliwaomba wananchi
kuendeleza ushirikiano ili kuimarisha huduma za nishati nchini na
kuhakikisha kuwa hakuna changamoto yoyote katika upatikanaji wa mafuta
nchini.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments :
Post a Comment